Na Denis chambi, Tanga.

WIZARA ya mifugo na Uvuvi  iko mbioni kuleta mradi wa kuwakopesha wafugaji Ng'ombe wa maziwa hapa nchini hii ikiwa na dhamira  Serikali ya kuwasaidia kuondokana na ufugaji wa mazoea ili waweze kupata faida zaidi.

Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua semina ya kuwapa elimu wafugaji wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga  iliyoandaliwa na  Wakala wa mafunzo ya Mifugo LITA kampasi 'BUHURI'  kwa lengo la kuwapatia njia bora ya kutumia katika kujihusisha na ufugaji wa kisasa ambapo amesisitiza ushirikiano baina ya wadau ,  wafugaji na serikali ili kuwezeaha kuinua zaidi sekta hiyo. 

Alisema wizara mifugo  na uvuvi inakuja na mradi mahususi wa kuwakopesha wafugaji  Ng'ombe  wa kisasa  wa maziwa ambao watatakiwa kulipa kupitia maziwa watakayozalisha  ambapo mchakato huo utakamilika hivi karibuni Mkoa wa Tanga ukiwa ni miongoni mwa wanufaika.

"Tuna mradi mwingine ambao unakuja  Muheza wa  'Climate smart Agricalture'  tunauita kopa Ng'ombe lipa maziwa ni mradi ambao kama mfugaji amekopeshwa Ng'ombe atatakiwa kurudisha maziwa  tukienda hivyo tutatoka haraka  bado tunamalizia mchakato wake na kwa bahati nzuri  kwa Mkoa wa Tanga upo kwenye mpango huu"

Adha amewataka wanufaika wa semina hiyo ambao ni wafugaji  kuzingatia mafunzo watakayopewa na kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo wakifuata maelekezo ili waweze kunufaika na ufugaji wa kisasa huku akiwataka wawezeshaji  kulitazama kwa karibu kundi la vijana wawe miongoni mwa wanaufaika ili kuweza kuwapatia ajira na hatimaye kuchangia pato la Taifa.

"Tuitumie fursa hii vizuri ili muweze kujikwamua kiuchumi inawezekana kama tukifuatilia haya maelekezo  na elimu ambayo tunapewa ufugaji ambao mnaufanya utasaidia kupata kipato lakini pia kupunguza utapiamlo" alisema Prof. Shemdoe.

 "Ili ufugaji wa hapa nchini uwe na tija na uwe endelevu ni vizuri kushirikiana kwa karibu na kundi kubwa la vijana serikali haiwezi kuajiri kila mtu lakini kujiajiri kwenye  maeneo kama haya ni rahisi niwaombe LITA na TALIRI kuweza kuliangalia hili la vijana" alisisitiza

Mkurugenzi wa TALIRI kanda ya Mashariki  Zabron Nziku alisema kuwa pamoja na kuwapatia wafugaji elimu bora ya namna ya kujikita kweye ufugaji wa kisasa bado wengi wao wamekuwa wakitumia wataalam ambao hawajulikani  hali ambayo imekuwa ikichangia kuwarudisha nyuma na kukosa faida huku akiomba elimu hiyo kuwafikia wataalam wa TALIRI na LITA.

"Tunatamani elimu hii pamoja na kuwapa wafugaji basi na wakufunzi kutoka LITA watafiti kutoka  TALIRI makao makuu waendelee kuelimishwambinu bora jinsi ufugaji utakavyoweza kuleta tija,  tulivyokuwa tukipita kwa wafugaji tumegundua kwamba wanao wataalam wengi wanaowatumia hawawajui kama wamethibitishwa na serikali na wamwkuwa wakilalamika kuwa matokeo wamekuwa hawayapati" alisema Nziku.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi meneja wa  wakala wa mifugo  LITA kampasi ya BUHURI William Moshi alisema  chuo kimekuwa kikitoa mafunzo ya aina mbalimbali ya muda mrefu na mfupi yakilenga kuwapa elimu  walengwa katika kujikita kwenye uzalishaiji wa maziwa kwa njia za kisasa,  ushauri elekezi na utafiti katik eneo la afya na uzalishaji wa mifugo.

Aidha ameongeza kuwa chuo hicho kimedhamiria kujenga kiwanda kidogo kwaajili ya kuchakata na usindikaji wa maziwa  ambapo kitasaidia kuongeza mnyororo wa thamani na kiwawezesha wafugaji kupata soko la uhakika wakati wote.

"Mteja wetu mkubwa wa maziwa yanayozalishwa  katika kampasi ya Buhuri ni Tanga Fresh hata hivyo bei yake ya maziwa ipo chini sana shilingi 800 na haiendani na  gharama za uzalishaji hivyo tunakusudia  kuanzisha  kiwanda kidogo cha usindikaji wa maziwa   ili kuongeza thamani ya maziwa tunayozalisha" alisema Moshi.

Aliongeza kuwa pamoja na shughuli nyingine kampasi hiyo image za miradi ya uzalishaji wa Ng'ombe wa mqziwa na nyama,  Nguruwe,  Mbuzi,  Kondoo  pamoja na kuku ambapo wamejuwa wakiwauzia wananchi waliopo jirani.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza    mkuu wa idara ya kilimo,  uvuvi na mifugo kayika wilaya hiyo Edward Mgaya alisema kuwa   elimu iyokuwa ikiyolewa mara kwa mara na BUHURI imekuwa na tija kwa wafugaji baada ya kuwasaidia na kuwawezesha vifaa mbalimbali ikiwemo vya usafiri ambapo amebainsiaha kuwa uzaliahaji wa maziwa katika wilaya hiyo umekuwa ni wa kiwango cha chini.

"Mafunzo haya ni ya Muhimu sana tunashukuru sana TALIRI kuona kuwa Muheza ni sehemu ya kuanzia mradi huu tumeshanza kuona manufaa tumepata pikipiki tisa kwa maafisa ugani na wamepata mafunzo wafugaji 72, mafunzo haya ni ya muhimu sana kwa wafugaji uzalishaji wetu ni mdogo sana tukiwatumia wataalam na kufwatilia mafuzo tunayopewa yatasaidia sana" alisema Mgaya.

Meneja wa  wakala wa mifugo  LITA kampasi ya BUHURI William Moshi akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi na utendaji wa chuo hicho katika kwenye semina iliyofanyika hivi karibuni mkoani Tanga.
Mmoja wa wafugaji na wanufaika wa mafunzo yanayotolewa na chuo cha Buhuri  akizungumza kwa niba ya wafugaji walioshiriki katika semina hiyo.

Share To:

ABDULLMAKAVELL

Post A Comment: