KATIKA kipindi cha miaka mitatu ya fedha 2021/22, 2022/23 na 2023/24 Serikali imejenga jumla ya vituo vya afya 466 vilivyogharimu Sh Bilioni 718.1 katika maeneo ya kimkakati kote nchini ambapo Mkoa wa Simiyu jumla ya vituo vya afya nane vimejengwa katika Kata za kimkakati kwa gharama ya Sh Bilioni nne.
Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu, Mhe Minza Mjika aliyehoji mkakati wa serikali wa kujenga vituo vya afya kwenye kata za pembezoni mwa Mkoa huo.
“ Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za kimkakati kote nchini zikiwemo kata katika Halmashauri za Mkoa wa Simiyu,” Amesema Mhe Dkt Dugange.
Post A Comment: