1000511740


Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, inaendelea kuifungua nchi kwa kujenga barabara za lami nchi nzima ili kufungua mkoa kwa nkoa na nchi jirani.

Kasekenya ameyasema hayo leo, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kibondo mjini (Nduta Junction-Kibondo town- Kibondo Junction Section -25.9km), inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi M/s Sinohydro Corporation Ltd, Mkoani Kigoma.

“Serikali inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha miundombinu ya barabara inajengwa vizuri kwa kuzingatia viwango, na moja ya sifa ya barabara zinazojengwa ni kuwa na viwango vya juu ili ziweze kudumu”, amesema Kasekenya.

1000511737


Aidha, amesema kukamilika kwa barabara hiyo, kutachochea fursa nyingi katika mkoa wa Kigoma na nchi jirani.

“Kwa watanzania ambao hawajapaona Kigoma, basi waje wapaone na waweze kuwekeza , kwa sababu sasa Kigoma inafikika kwa lami toka mikoa yote na tunaenda kukamilisha barabara ya kutoka Kasulu kwenda Mwanza, na barabara ya Kigoma kwenda Dodoma wakandarasi tayari wapo Site” amesema Kasekenya.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini ( TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, amesema wanaendelea kumsimamia mkandarasi kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati.

Naye Mhandisi wa Mradi, Eng. Hatibu Kapombe, amesema barabara hii imefikia asilimia 63.1 na inatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2024,na mkandarasi anaendelea na kazi usiku na mchana.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali, Isaac Mwakisu ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan chini ya Wizara ya Ujenzi, kwa kuleta maendeleo katika mkoa wa Kigoma kwani barabara nyingi ni zimejengwa kwa kiwango cha lami na zinapitika wakati wote.
1000511743
Share To:

Post A Comment: