MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC),Dkt.Benson Ndiege,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti kwa vyama vya ushirika lililofanyika leo Januari 11,2024 katika shule ya msingi Uhuru jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

ZOEZI la upandaji miti kwa vyama vya ushirika limezinduliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia ili kukabilina na mabadiliko ya tabianchi.

Uzinduzi huo umefanywa leo Januari 11,2024 na Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC),Dkt.Benson Ndiege, baada ya kupanda miti katika shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma.

Dkt.Ndiege, amesema kuwa suala la mazingira ni ajenda ya kidunia ya kuhakikisha wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Tumeamua kumuunga mkono Rais wetu pamoja na viongozi wengine ambao wamekuwa wakituhamasisha kuhusu suala zima la utunzaji wa mazingira katika upandaji Miti hasa kwenye msimu wa Mvua sisi Tume tunaahidi kufuata nyayo zao,"Amesema Dkt,Ndiege

Mrajisi huyo,amefafanua kuwa kupitia vyama vya Ushirika ambavyo vina mashamba viendelee kupanda miti kwenye taasisi za umma, shughuli za ushirika ni shughuli za kiuchumi.

"Asilimia 60 ya vyama vya ushirika ni vya kilimo na ili kuwa na kilimo chenye ustawi lazima kulinda mazingira, kwani kkkwenye vyama vya ushirika vya mifugo kukiwa na ukame inasabaisha ukosefu wa malisho ya mifugo.”amesema

Aidha Dkt.Ndiege,amesema kuwa Tume hiyo inasimamia vyama vya ushirika nchini na vilivyopo hadi sasa ni 7400 na zoezi hilo litafanyika nchi nzima.

“Wanaushirika wanapaswa kulinda na kutunza mazingira ili kuimarisha uchumi, kama mlivyoona tuna uwakilishi hapa wa vyama vya ushiriki na tunakopa ili tukawekeze kwenye kilimo, mifugo na uvuvi kwenye mazingira mazuri,”amesisitiza.

Kwa upande wake Mtendaji wa SACCOS ya Mamlaka ya kusimamia ununuzi wa umma Bi.Janeth Kalinga amesema kuwa wanaahidi kutekeleza mkakati huo wa upandaji miti katika chama chake cha akiba na mikopo ili kulinda mazingira kwa vizazi vijavyo.

Naye, Ofisa Mistu daraja la pili kutoka Wakala wa Misitu (TFS), Leonard Bilomo,ameipongeza Tume hiyo kwa juhudi hizo na kusisitiza kusimamia miti hiyo inayopandwa itunzwe na kukua.
WANAFUNZI wa Darasa la tano Shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma wakiwa wamebeba miti kwa ajili ya kupanda.
MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)
,Dkt.Benson Ndiege,akipanda mti katika shule ya msingi Uhuru jijini Dodoma mara baada ya kuzindua zoezi la kupanda miti kwa vyama vya ushirika leo Januari 11,2024.
MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)
,Dkt.Benson Ndiege,akimwangilia Maji mti katika shule ya msingi Uhuru jijini Dodoma mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti kwa vyama vya ushirika leo Januari 11,2024.
WATUMISHI wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru wakipanda miti mara baada ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ,Dkt.Benson Ndiege kuzindua zoezi la kupanda miti kwa vyama vya ushirika leo Januari 11,2024 jijini Dodoma.
MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)
,Dkt.Benson Ndiege,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti kwa vyama vya ushirika lililofanyika leo Januari 11,2024 katika shule ya msingi Uhuru jijini Dodoma.
MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)
,Dkt.Benson Ndiege,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti kwa vyama vya ushirika lililofanyika leo Januari 11,2024 katika shule ya msingi Uhuru jijini Dodoma.
WANAFUNZI wa Darasa la tano Shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma wakiipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kwa kupanda miti katika shule hiyo.
Ofisa Mistu daraja la pili kutoka Wakala wa Misitu (TFS), Leonard Bilomo,akizungumza mara baada ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kupanda miti katika shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma.
Mtendaji wa SACCOS ya Mamlaka ya kusimamia ununuzi wa umma Bi.Janeth Kalinga,akitoa aahadi kutekeleza zoezi hilo la upandaji miti katika chama chake cha akiba na mikopo ili kulinda mazingira kwa vizazi vijavyo.
MRAJIS wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)
,Dkt.Benson Ndiege,akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Darasa la tano Shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti kwa vyama vya ushirika lililofanyika leo Januari 11,2024.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: