Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Danielson Palangyo, Akabidhi Miche Elfu Ishirini na sita mia tatu ( 26,300) za kahawa ,kwa wananchi na Wakulima wa kijiji cha Ngyani Kata ya Ngwaranga jimboni hapo kwa lengo la kufufua Chama Cha Usharika wa Mazao Ngyani.
Ukabidhishwaji wa miche hiyo imetekelezwa na Mbunge wa Jimbo hilo katika Viwanja vya Usharika wa mazao Ngyani na kusema hiyo itasaidia uchumi wa mtu mmoja mmoja kukua kwani zao hilo huuzwa kwa Dola.
"Uchumi wa Meru ulianguka wakati tuliacha kulima Kahawa sikujua kama itafikia hatua hii lakini wananchi wa Meru hali yao kiuchumi ni mbaya sana , na simaanishi kilimo cha nyanya au viazi sio kilimo hapana ni kilimo cha msimu ambacho inafika hatua mazao yanauzwa kwa bei ya hasara, kwa hiyo mwaurobaini wa Meru ni kurudi katika kilimo cha kahawa, turudi kwenye uchumi ambao tulikuwa nayo ,leo nakabidhi miche zaidi ya elfu 26 na niseme zoezi hili ni Endelevu" alisema Palangyo
Kwa Upande wake Elishilia Mathayo Njeve balozi wa zao la Kahawa Meru, Amethibitisha kupokea miche hizo elfu 26 za kahawa ambayo ni miche bora haipati kutu, ambapo mche mmoja huvunwa kilo hadi kilo 10 kavu za kahawa,huku kilo moja ikiuzwa kwa shilingi elfu tano (5).
" Ina maana kwa leo mbunge ametupatia miche yenye thamani ya shilingi Billioni 330 elfu , Ambayo ni uchumi utakaokuwepo hapa Meru na kama halmashauri nao watachukua yao watapata millioni 53 na laki 2 kwa hiyo uchumi wa Meru utapanda, Mpango wetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali ili pia hata usharika wetu uweze kuwa wa kisasa na hata mashine zetu za kumenyea kahawa ambazo ni za siku nyingi sana 1957 tuweze kupata za kisasa".Alisema Elishilia
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wengine na wakulima wa kijiji cha Ngyani Joshua Ayo na Gladness Ayo ,wamesema chanzo cha wao kusimamisha kilimo cha kahawa ni kutokana na soko kuyumba, ila kwa sura ya mbunge ya kuwakabidhi miche leo wamekiri kufufua zao kwa kushirikiana na viongozi wa usharika pamoja na viongozi wa eneo hilo.
Post A Comment: