Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro
Mbuge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango amechangia kiasi shilingi Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Mtundu iliyopo kata ya Mahole wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Amesema mchango huo ni kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake akisema shule za aina hiyo zinazohitaji ujenzi zipo nyingi kwenye Jimbo hilo na tayari baadhi zimekamilika na kuanza kutumika.
Amesema fedha hizo zitasaidia kuanza ujenzi wa Madarasa Matatu na ofisi kwenye shule ya Msingi Mtundu na Serikali kuu imehaidi kusaidia ujenzi huo ili kuwesesha madarasa hayo kukamilika kwa wakati.
Aidha amewapongeza wananchi wa kata ya Mahole kunakofanyika ujenzi huo kwa juhudi binafsi katika nyanja mbalimbali za maendeleo hasa eneo la elimu Kwa kujitolea michango na nguvukazi kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha watoto wote wanapata haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupata Elimu kwenye mazingira rafiki ikiwemo Miundombinu.
"Ninapozungumza tayari wananchi hawa kwa nguvu zao wameanzisha ujenzi wa Msingi wa Madarasa mawili kwa hatua za maandalizi ya awali bila kusubiri serikali". alisema Mhe. Kilango.
Mbali ya mchango huo Mhe. Kilango aliwatia moyo wananchi hao kuendelea na mshikamano kwa kuhakikisha wanasonga mbele katika kufanikisha shabaha iliyopo ya ujenzi wa ofisi na madarasa Matatu ya Shule ya Mtundu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mahole Issa Rashid amempongeza Mhe. Kilango kwa jitihada zake kupambania miradi ya Maendeleo na Ile ya kuboresha huduma ikiwemo ujenzi wa shule hiyo ambao umeongeza ari kwa wananchi kujitolea.
Mhe Kilango akikagua Madarasa ambayo yenye nyufa Mbalimbali pia siyo Rafiki kwa watoto kusoma kwenye Madarasa hayo hasa kipindi hichi cha mvua ambazo zinazoendelea kunyesha Nchi zima
Mwisho
Post A Comment: