📌Wajiuliza mradi umefanikiwa vipi

📌Wakusanyika kupiga picha kwenye Bango

Watu wengi Mjini Unguja,Zanzibar wamejitokeza kutembelea Banda la TANESCO katika viwanja vya Fumba ambapo Maonesho ya 10 ya kimatafa  ya Biashara yanafanyika .

Maonesho hayo yaliyoanzaTarehe 7 January 2024, yameleta Taswira mpya ya wadau wa Umeme juu ya jitihada ambazo Serikali inazifanya kwenye uwekezaji wa Sekta ya Nishati Nchini.

Mmoja ya wadau aliyetembelea Banda hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Mhe. Selestine Kakele ambae ameonekana kuvutiwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na hasa mradi wa JNHPP ambao umefikia asilimia 95.83

Naye Bw. Mwangulumba Mtumishi katika Bodi ya Taifa ya Pamba,Tanzania amesema kuwa mradi wa JNHPP ni tumaini Jipya kwa Tanzania na kuwa utekelezaji wake umekua wa kipekee sana kwani ni mradi uliopitia changamoto nyingi sana hasa kutoka katika Mataifa makubwa yaliyoendelea lakini Tanzania imeonesha uthubutu.

“ najiuliza tumewezaje kulifanya hili, huu mradi wa kipekee , maono ya waasisi wetu yalikua makubwa sasa hata wale ma Giant  wanatushangaa, hili tumeliweza” 

Naye Bw.Issa Waziri mkazi wa Pemba, amesema kuwa mradi wa JNHPP si tu utatupatia umeme wa kutosha lakini umekua kivutio kwa namna unavyoonekana

“Mradi huu ni mzuri sana, kwanza unavutia, umeshawahi kufika (akiongea na mwandishi)natamani sana kufika hapo”

Shamra shamra za Maonesho haya zimekua za kihistoria kwa TANESCO na hasa kwa baadhi ya watu kuja na kupiga picha katika moja ya bango la Mradi wa JNHPP.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: