Na John Walter-Manyara.

Wizara mbalimbali za kisekta zimeendelea kuratibu zoezi la uokoaji katika  kubaini chanzo Cha maafa katika mlima Hanang ulioko wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa jana Tarehe 4.12.2023 amehibibitisha vifo 63 , ikiwa wanaume 23 na wanawake 40 pamoja na majeruhi 116.

Majeruhi hao ikiwa ni wanaume 56 na wanawake 60 vilivyotokea kwenye maafa ya mafuriko Hanang. ambapo aliwasilisha pole za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wana Manyara na watanzania.

Mamia ya watanzania wamehudhuria ibada  maalum katika viwanja vya shule ya msingi Kateshi eneo mojawapo lililowahifadhi wahanga wa mafuriko kupokea miili ya ndugu zao tayari Kwa maziko ikiwa ni maelekezo ya  Rais kuwa huduma za miili yote itafanywa na serikali kwa kupewa majeneza na kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Cuthbert Sendiga ameshukuru serikali  kuungana na wana Hanang kusaidia wahanga.

" Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan tunamshukuru kwa namna ambavyo amelikimbilia na kuchukua jambo la wenye maafa kama jambo lake kwa kuelekeza vyombo mbalimbali pamoja na serikali kufika Hanang,Tunashukuru" Amesema Sendiga.

Amesema eneo kubwa lililoathirika na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi katikati ya mji wa Katesh.na kwamba Serikali imeongeza juhudi za kufukua vifusi kuondoa miili katika tope zito Ili  kurejesha miundo mbinu katika hali yake ya kawaida.

Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jumapili imesababisha mafuriko ya tope zito katika eneo hilo

Share To:

Post A Comment: