Na John Walter

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amewataka wataalamu wa ardhi kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa vijiji taratibu za upangaji na upimaji wa ardhi.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo Wilayani Musoma mkoa wa Mara wakati akiongea na Viongozi wa Kamati ya Usalama wa mkoa na maafisa wa sekta ya ardhi katika ziara yake ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Vijiji 975 nchini.

Waziri Silaa amewapa muda huo wa miezi sita (6) wataalamu wa ardhi katika wilaya zao nchi nzima ili kuhakikisha wanawafundisha wananchi na viongozi wa vijiji maana ya upangaji na upimaji wa viwanja na kuwapa uelewa ili kuepuka upangaji holela wa vijiji.

Amesema kazi hiyo haihitaji gharama kwani ni suala la elimu ambalo linaruhusiwa kutolewa katika mikutano ya wenyeviti wa vijiji na kuwaelekeza maana ya upimaji wa awali wa viwanja na mashamba.
Share To:

Post A Comment: