Waziri wa katiba na sheria Balozi Dkt. Pindi Chana amezindua kamati ya Kitaifa ya mpango kazi wa haki za binadamu na biashara na kuitaka kamati hiyo iharakishe mapitio kwa ajili ya kuleta tafsiri halisi ya haki katika kuwezesha biashara na uwekezaji ikizingatia masuala ya ardhi.

Akizindua kamati hiyo Jijini Arusha Balozi Dkt, Pindi Chana amesema bado kuna changamoto katika sekta hiyo hususani masuala ya biashara na ardhi jambo linalopaswa kufanyiwa mapitio ili kuleta mageuzi ya haraka ya katika uchumi wa Nchi..

Alimpongeza mwenyekiti wa  tume ya haki za binadamu ikiwemo kuendelea kukuza misingi na kanuni za haki za binadamu na biashara kwani Rais Samia Hassan Suluhu amefungua mipango ya fursa za kibiashara ikiwemo uwekezaji.

"Biashara kuanzia ngazi za vijiji,kata na matawi lazima haki za binadamu zilindwe ili kuhakikikisha biashara zinakuwa ikiwemo haki za binadamu kuzingatiwa"

Alisisitiza kuwa wizara hiyo itakuwa bega kwa bega na kamati hiyo ili kuhakikikisha biashara na mipango mkakati inyaowekwa na kamati hiyo ikamilike ili kuhakikikisha mpango waliyojiwekea inakwenda kwa wakati.

 



Share To:

Post A Comment: