Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme, leo tarehe 8 Disemba 2023.
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo pamoja na maeneo mbalimbali nchini.
Miundombinu hiyo iliyoharibiwa na mvua ni pamoja na barabara ya Shinyanga - Old Shinyanga, barabara ya Old Shinyanga - Solwa, barabara ya Solwa - Kahama na miundombinu mingine ya barabara katika mkoa huo.
Post A Comment: