Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imetoa mafunzo ya masuala ya kijamii na Mazingira kwa watumishi wa Halmashauri 12 zinazotekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa TACTIC unaotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya Dunia.
Mafunzo yamefanyika mkoani Morogoro na kuhudhuria na washiriki 75 wakiwemo wataalamu wa masuala ya Kijamii na mazingira kutoka kwa mtaalamu mshauri na mkandarasi lengo likiwa ni kuhakikisha miradi inayotekelezwa haileti athari za kimazingira na kijamii katika halimashauri hizo.
Mratibu wa Mradi TACTIC kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Emmanuel Manyanga amewakumbusha wataalamu hao kuhakikisha wanasimamia na kuondoa athari za kijamii na kimazingira wakati wa kuelekea utekelezaji wa mradi huo.
Kadhalika,Mtaalamu wa masuala ya kijamii na mazingira kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Beatrice Mchome ameshauri malipo ya fidia ya ardhi kwa wamiliki wa awali wa maeneo yanayotekekeleza mradi kabla ya kutangaza eneo la uwekezaji.
Post A Comment: