Pic-3-2-1024x683

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mimea Tiba (kulia) alipotembelea Maabara ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, wakati wa ziara ya kikazi Disemba 14,2023 jijini Arusha.

...............

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo ameipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kuzalisha wataalam wabobezi 213 ambao ni walimu katika Vyuo Vikuu mbalimbimbali nchini na kusisitiza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kuendelezwa zaidi ili kusaidia kuleta maendeleo katika tafiti, ujenzi wa maabara za kisasa na mifumo ya undeshaji.

Profesa Carolyne ameyasema hayo Desemba 14, 2023 katika ziara ya kikazi kwenye taasisi hiyo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbimbali zinazofanyika hususani katika masuala ya tafiti na bunifu.

“shirikianeni na wataalam wabobezi katika sekta ya biashara ili muweze kutatua changamoto za ajira na kutoa fursa za ukuzaji uchumi unaotokana na tafiti za masoko ya ndani na nje ya nchi” alisema Professa Carolyne Nombo.

Aliongeza kuwa, wataalamu hao watasaidia kutatua changamoto za teknolojia kubwa ikiwemo biashara ili kukuza uchumi na kusaidia vijana kupata ajira kutokana na kupata fumbuzi ya aina ya biashara wanazopaswa kufanya, masoko, kujua faida na hasara pamoja na utunzaji wa kumbukumbu.

"Lazima sasa wataalam wabobezi wa sayansi na teknolojia muwekeze zaidi katika biashara ili vijana wajue changamoto za biashara zipoje watakapoingia sokoni " amesisitiza Professa Carolyne

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi , Profesa Maulilio Kipanyula alisema taasisi hiyo ni mojawapo ya taasisi inayotoa gunduzi za kisayansi na teknolojia ikiwemo utoaji wa matokeo ya tafiti kwa manufaa ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi ,Taaluma,Tafiti na Bunifu ,Profesa Anthony Mshandete alisema taasisi hiyo ina jumla ya wanafunzi 593 pamoja na programu 33 lakini pia inafanya tafiti mbalimbali ikiwa ni maono ya kufikia malengo makubwa zaidi ya kitafiti na maendeleo katika masuala ya bunifu, tenknolojia ili kasi ya maendeleo ya tenknolojia iendane na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi zikiwemo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).

Pic-1-2-1024x683

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (kulia) akiongea na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (hawapo katika picha), wakati wa ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14,2023 jijini Arusha, Kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula.

Pic-2-2-1024x854

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo(kulia) akiongea na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, katika ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14, 2023 jijini Arusha.

Pic-3-2-1024x683

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mimea Tiba (kulia) alipotembelea Maabara ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, wakati wa ziara ya kikazi Disemba 14,2023 jijini Arusha.

Pic-4-2-1024x683

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (wa kwanza kulia) akipata maelezo kuhusu utafiti wa funza lishe kutoka kwa Mtafiti Bi. A kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Computer) ziza Konyo (Kushoto) alipotembelea Kituo cha Atamizi (Incubation Centre) wakati wa ziara ya kikazi Disemba 14,2023.

Pic-5-2-1024x683

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo(katikati) akipata maelezo kuhusu kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data kwa kasi kubwa (Param Kilimanjaro Super Computer) kutoka kwa Afisa Tehama Bw. Mdoe Mwamunyange (Kulia), wakati wa ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14,2023 jijini Arusha, Kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula.

Pic-6-1024x683

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa Carolyne Nombo (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela , wakati wa ziara ya kikazi katika Taasisi hiyo Disemba 14,2023 jijini Arusha.

Share To:

Post A Comment: