1000457854


Na Issa Sabuni na Beatrice Lyimo

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ametoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya umeme vijijini ili iendelee kuwa na thamani kwa sasa na vizazi vijavyo.


Mhe. Kapinga ametoa wito huo  katika Kata ya Makuyuni iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini mkoani Tanga wakati akikagua Mradi wa Kupeleka Umeme Awamu ya Tatu, Mzungungo wa Pili, unaotekelezwa na mkandarasi, kampuni ya Tontan Ltd chini ya usimamizi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).


“Ninaendelea kuwaomba, mlinde miundombinu ya miradi hii kwani miradi hii ni ya thamani kubwa, tuoneshe ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi hiyo kwani miradi hii haina fidia na inagharamiwa kwa fedha nyingi, ikiwa na lengo la kupeleka huduma kwa wananchi hivyo niwaombe kutoa ushirikiano ili miradi isichelewe, kama eneo lako litatakiwa kupita nguzo toa ushirikiano kwa kuwa umeme unaopita hapo hauna madhara” ameeleza Mhe. Kapinga


1000457840

Aidha, Mhe. Kapinga amebainisha kuwa, Serikali itaendelea kuleta fedha katika jimbo hilo la Korogwe vijijini na itazidi kusimamia miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili wananchi wote wapate huduma ya umeme.


Pia amesema, Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili iwanufaishe wananchi kama ilivyopangwa.
Mbali na hayo, Mhe. Kapinga amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kutenda haki kwa wananchi kwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati kwani kulegalega kwao kunakwamisha maendeleo kwa wananchi hao.


1000457848

Kwa upande wake Msimamizi wa miradi ya REA mkoa wa Tanga Mhandisi Balisidya Myula amebainisha kuwa Jimbo la Korogwe Vijijini lina Jumla ya Kata 29, Vijiji 118 na Vitongoji 610 ambapo vijiji 91 sawa na asilimia 77% vilipatiwa huduma ya umeme kupitia Miradi ya REA III (Mzunguko wa Kwanza na wa Pili) hivyo vijiji 27 ambavyo havina umeme vinataraji kuunganishwa na huduma ya umeme kabla ya Mwezi Juni, 2024.


Akizungumzia Mradi wa REA III (Mzunguko wa Pili) katika Kijiji cha Sharaka, Mhandisi. Myula amesema Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 151.5 na mkandarasi (Kampuni ya Tontan Ltd) umekamilika kwa asilimia 80 na kazi iliyobaki inatarajiwa kumalizika ifikapo Tarehe 31 Desemba, 2023.


Mhandisi Myula ameitaja Miradi mingine inayotekelezwa katika Jimbo la Korogwe vijijini kuwa ni pamoja na Mradi wa Kupeleka Umeme kwenye Migodi Midogo na Maeneo ya Kilimo; Mradi wa Kupeeka Umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji na Mradi wa PERI Urban III.


Nae Msimamizi wa Miradi kutoka kampuni ya Tontan Ltd, Mhandisi, Lomayan Mollel amewaomba radhi wananchi wa kijiji cha kwa kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo na kuahidi kuwa mradi huo utakamilika ifikapo desemba 31, 2023


“Ninaomba radhi kwa wananchi kwa kuchelewesha huduma hii ya kupatikana kwa umeme katika kijiji cha Makuyuni, ninaahidi Mradi huu utakamilika, ifikapo Desemba 31, 2023 kwani kwa sasa, tupo hatua za mwisho za ukamilishaji”. Ameeleza Mhandisi Mollel.


Serikali kupitia REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza nishati ya umeme vijijini ambapo Wakala umeendelea kutekeleza Miradi mbalimbali katika Jimbo la Korogwe vijijini, ikiwa na lengo la kuwapa wananchi huduma bora ya nishati ili kuboresha huduma za kiafya kijamii na maendeleo ya kiuchumi vijijini.
IMG-20231206-WA0054
IMG-20231206-WA0048
IMG-20231206-WA0053
IMG-20231206-WA0051
IMG-20231206-WA0049
IMG-20231206-WA0052
IMG-20231206-WA0055
IMG-20231206-WA0057
IMG-20231206-WA0058
IMG-20231206-WA0075
IMG-20231206-WA0076
Share To:

Post A Comment: