Na John Walter-Manyara
Uongozi wa chama cha wafanyabiashara ndogondogo kutoka Soko Kuu la Babati wamekabidhi misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea mlima Hanang’ Mkoani Manyara Disemba 3, 2023.
Wafanyabiashara hao wamekabidhi bidhaa za jikoni ikiwemo nyanya, matunda, mboga za majani, nguo, sabuni na pesa kiasi cha Shilingi laki moja.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao, kiongozi wa umoja huo maarufu kwa jina la mama Singida alitoa salamu za pole pamoja na kukabidhi misaada iliyopokele na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi katika Ofisi Halmashauri ya Hanang’ mkoani Manyara.
Akitoa neno la shukran Katibu Mkuu huyo amewapongeza wafanyabiasha hao kwa kuona umuhimu wa kujitolea na kutoa vitu vitakavyosaidia mahitaji ya waathirika hao huku akiendelea kuwaomba wadau kujitokeza zaidi
“Kipekee ninawashukuru sana, hili ni jambo jema kuwakumbuka wenzetu walipata maafa haya, na misaada yenu itawafaa sana hususan masuala ya chakula na viungo vya jikoni, mmefanya vyema sana,” alisema Dkt. Yonazi
Post A Comment: