Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Dr John Danielson Pallangyo akiwa katika mwendelezo wa ziara zake kwenye Jimbo za kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo , Leo Amefanya ziara katika kata ya Shambarai Burka kukagua miradi ya maendeleo sambamba na kuwatembelea Wahanga wa Mafuriko waliokumbwa na janga hilo lililosababisha takriban Kaya 15 kuharibiwa makazi yao na Hekari Takriban elf tatu (3).
Ziara hiyo ya mbunge John Danielson Pallangyo Maarufu John D iliambatana pia na kutembelea shule ya sekondari Ya kata ya Shambarai Burka na kusikiliza kero na changamoto katika shule hiyo iliyoambatana na utoaji wa mitungi ya Gesi kwa wananchi walioharibiwa makazi yao kufuatia Mafuriko pamoja na Walimu wa Shule hiyo, na kusema lengo la kutoa mitungi hiyo kwanza ni kuhimiza kampeni ya utumiaji wa gesi kwa lengo la kupinga ukataji wa miti nchini hususani katika taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii kama Mashuleni, Hospitalini, vituo mbalimbali na hata kwa watu mmoja mmoja.
Kata ya Shambarai imepata fedha nyingi za miradi ikiwemo;- Ths Milion 120 ujenzi wa madaraja mawili ya kuunganisha kata na vijiji Tsh Milion 100 ujenzi wa zahanati,Tsh Milion 27 uchimbaji wa kisima cha maji,Tsh milion million 40 ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya Sec Shambarai Burka,Tsh milion 3 mfuko wa jimbo kwaajili ya ukarabati wa shule ya sec Shambarai Tsh Milion 60 kwaajli ya kuweka Vilula (stand za kutolea maji) kwenye kijiji cha Shambarai!Na fedha nyingine zinaendelea kuja kwaajili ya kutatua kero na changamoto za wananchi.
Aidha kwa upande mwingine Mkuu wa shule ya Sekondari Shambarai Burka Bi AZIZA MAULIDI SIMBA ,amesema changamoto kubwa katika Shule hiyo ni eneo la shule kuwa dogo, upungufu wa madarasa, Matundu ya vyoo, Nyumba za walimu, Jengo la Utawala Ambapo Changamoto hizo zote alizielekeza kwa mbunge Dr John D ,Ambapo mbunge huyo alizipokee na kuahidii kufanyia kazi kwa haraka.
Wakizungumza baadhi ya waathirika wa mafuriko hayo baada ya kukabidhiwa Msaada huo wa mitungi , wamesema wamekuwa wakipitia changamoto hasa katika kupika kutokana na kwamba kuwa na asilimia kubwa ya matumizi ya kuni , ambapo kuafuatia mafuriko wameethirika kwa asilimia kubwa kuni kunyeshewa ila kupitia msaada wa mitungi hiyo watakuwa na uhakika wa kupata chakula.
Aidha kwa Upande wake Diwani wa kata hiyo Bwana John Mollel Amesema wananchi walioathiriwa na mafuriko ni zaidi ya elfu moja (1), Lakini waliopoteza makazi ni takriban kaya 15, Pamoja na mashamba Hekari elfu tatu (3).
Post A Comment: