Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi nguvu za pamoja na harakati, kutoka TGNP, Florah Ndaba akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2023 na Wanaasasi za Kiraia kutoka mikoa tofauti tofauti hapa nchini juu ya mfumo ambao Mashirika yasiyo ya kiserikali kuweka taarifa zao na kazi zao wanazozifanya katika jamii juu ya kutetea haki za Wanawake, wasichana na watu waliopembezoni ili jamii ione.






Baadhi ya wadau wakiwa katika mafunzo ya jinsi ya kuweka taarifa za Asasi zao za kiraia katika mfumo.

KATIKA Kutekeleza Mradi wa Pamoja Tapo sauti ya Mwanamke na Uongozi Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) watoa elimu kwa vitendo juu ya Mfumo wa taarifa za Asasi za kiraia.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi nguvu za pamoja na harakati, kutoka TGNP, Florah Ndaba jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2023 amesema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wamiliki au wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kuweka taarifa zao pamoja na kazi mbalimbali wanazozifanya ili kuleta maendeleo katika utetezi wa kazi za mwanamke, msichana na watu waliopembezoni.

Amesema kuwa kupitia Mradi huo unafanywa na Mashirika Mawili ambayo ni Women Fund Tanzania na TGNP ambao unafanywa katika Mikoa 10 ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Lindi, Mtwara, Dodoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Kigoma na Mara.

Lengo kuu la Mradi huo ni kuhakikisha wanawake na wasichana na watu walio pembezo wanafaidika na wanafurahia haki za binadamu na haki zao.

Frolah amesema wakati wanaanza mradi huo kulikuwa na maeneo yenye changamoto kwa nchi ambayo waliyaibua, maeneo hayo ni ushirikiano wa pamoja baina ya watetezi wa haki za wasichana na Wanawake ambao wanapelekea kufanya mabadiliko ambayo yanapekekea wanawake na wasichana na watu waliopembozoni kufurahia haki zao.

"Tunajua ili watu wafurahie haki kunawafadhili wengi ambao wanatakiwa washirikishwe ikiwemo Asasi za kiraia zinazofanya kazi ya kutetea haki za wanawake lakini pia tuligundua kuwa na changamoto ya taarifa za jinsi ya Asasi za kiraia zinafanya kazi."

Kwa hiyo mfumo huo ulitengenezwa kwaajili ya kusaidia Asasi za kiraia hasa zisizo na uwezo mkubwa wa kujiendesha, ingawawanafanys kazi katika ngazi ya jamii.

Amesema Asasi hizo zilikuwa hazina uwezo wa kuonesha ushahidi wa kazi wanasozifanya kutokana na kutokuwa na uelewa wa kufungua tovuti na mitandao ya kijamii. Ila kwa sasa Teknolojia imeenea tunaona inawezekana ndio maana tumekuja na programu ya pamoja kwaajili ya kuweka taarifa za kila Shirika.

Akizungumzia kuhusiana na mashirika ambayo yamejisajili TGNP na yameshaingia katika mfumo hio, Frolah amesema kuwa mashirika 100 ya mfano yameshaingiza taarifa zao katika mfumo huo ingawa Mtandao huo umesajili Asasi za kiraia 260.

Amesema kazi kubwa ya Programu hiyo nikuonesha kazi za Asasi za Kiraia lakini kuonesha nguvu iliyopo katika maeneo tofautitofauti kwa sababu itakuwa Programu moja inayoonesha Asasi za Kiraia kuona zinaonesha mambo makubwa wanayofanya.

Pia ni amesema kuwa Asasi za Kiraia zinazoweka taarifa zake katika mfumo huo zitakuwa zinatoa ushahidi wa kazi ambazo wanazinafanya katika maeneo yao.

"Pia ni njia mojawapo ya fundruising tool pale wanapotaka kufanya kazi zao na zionekane kupitia mfumo huo." Ameeleza Florah

Amesema kubuni mfumo huo ilikuwa ni kuwasaidia mashirika kuonesha kazi zao lakini kuyasaidia mashirika kuwapa uelewa juu ya umuhimu wa kukusanya taarifa, kwa sababu walikuwa hawana uelewa wakukusanya taarifa ambazo zinatakiwa kusambazwa kwa jamii ili jamii ione
Share To:

Post A Comment: