1000461575

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amesema mamlaka inaweka mfumo sahihi utakaohakikisha mbolea za msaada kwa waathirika wa mafuriko Wilayani Hanang zinawafikia walengwa.

Amesema taarifa za wakulima waliojisajili katika eneo lililoathiriwa zipo na kutoa wito kwa wale ambao bado hawajajisajili kufanya hivyo ili kupata mbolea hizo.

Laurent ameeleza hayo leo tarehe 8 Desemba, 2023 kwenye kituo cha kilimo alipokuwa akifanya makabidhiano maalum na Kamati ya Maafa kupitia Afisa Kilimo wa Wilaya ya Hanang, Liberatus Msasa.

1000461596

Amesema ofisi ya Kilimo wilayani Hanang itashirikiana na Ofisi ya Mamlaka kanda ya Kaskazini kuhakikisha Afisa Kilimo anasajiliwa kama wakala na kuingiziwa mbolea hizo kwenye accounti yake ili aweze kuzigawa kwa waathirika bure kwa utaratibu uliowekwa.

Amehitimisha mazungumzo yake kwa kutoa pole kwa waathirika wote na kuwaombea majeruhi warejee katika hali zao za kawaida na wale waliotangulia mbele ya haki pumziko la amani.

1000461593

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Ndani na Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja wa TFRA, Louis Kasera ametoa shukrani kwa wadau wote waliochangia na kuwezesha kupatikana kiasi cha tani 78.5 za mbolea.

Amesema kiasi hicho kitawasaidia waathirika kuendelea na shughuli zao za kilimo pasipokuwa na shida kwani watapokea mbolea za kupandia na kukuzia.

Naye, Afisa Kilimo wa Wilaya ya Hanang, Liberatus Msasa, ameshukuru kwa msaada huo na kueleza wilaya yake unategemea kilimo kwa asilimia 80 na kueleza sekta hiyo imeathiriwa na janga hilo.

Ameahidi kusimamia ugawaji wa mbolea hizo na kuhakikisha walengwa ndio wanaonufaika na pembejeo hiyo muhimu.
1000461587
1000461584
1000461572
1000461581
1000461590
Share To:

Post A Comment: