Na John Walter-Manyara

Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania  (TANAPA) limetoa kikosi cha askari wake 19 na kiongozi mmoja  kuungana na vikosi vingine vya majeshi vilivyopo katika eneo  lilopata maafa ya maporomoko ya  mawe na miti wilayani Hanang' Mkoa wa Manyara.

Lengo la kikosi hicho ni kusaidia kutoa utaalamu  katika  uokoaji na kurejesha haraka hali ya miundombinu ya mji huo.

Kaimu kamishna wa uhifadhi (TANAPA) Mussa Kuji amesema maafa yaliyotokea yamepoteza nguvu kazi ya Taifa na kuleta huzuni Kwa watu kufuatia kupoteza ndugu,wazazi na watoto.

"Napende kutoa pole kwa Jamii ya Katesh Kwa maafa ambayo hayakutegemewa maafa ambayo yamegharimu watu wengi na kuacha watu hao wakiumia na kupoteza wapendwa waoTANAPA inawafariji". Alisema

TANAPA imetoa mashine ya kusaidia shughuli za uokoaji, na shilingi Milioni kumi.
Share To:

Post A Comment: