Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya maafa iliyotokea tarehe 2/12/2023 Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara kufuatia mvua kubwa iliyopelekea mafuriko na Mawe makubwa na Miti kutoka Mlima Hanang kuporomoka na kuingia mji wa Kateshi na kusababisha athari kwa kaya 1,150 na watu 5,600, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na majeruhi 80 ambao wamepelekwa hospital mbalimbali.
Natoa pole kwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan,Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndugu ,jamaa na marafiki walioguswa na misiba hiyo na nawaombe Marehemu wapumzike mahala pema Peponi na majeruhi wote wapone haraka,pia natuma salam za pole kwa wananchi wote waliokumbwa na maafa hayo.
UWT inapongeza Juhudi za Serikali kwa hatua mbalimbali za haraka zilizochukuliwa kutokana na maafa haya,ikiwemo msaada wa dharura na uokoaji, kuwapatia makazi na kugharamia matibabu kwa waathirika.
Aidha sisi UWT tunaiunga Mkono Serikali kwenye jitihada hizo na leo tarehe 4/12/2023 jiji Dar Es Salaam imefanyika Kamati ya Utekelezaji ya Dharura ambayo imewaalika wajumbe wa Baraza Kuu waliopo Dar Es Saalam,wabunge wa Viti Maalum na baadhi ya viongozi na tumejipanga kwenda Hanang haraka kuwafariji wananchi wenzetu waliofikwa na maafa haya na kwenda kukabidhi vifaa mbalimbali ambavyo UWT kwa kushirikiana na wadau wetu tumefanikiwa kuvinunua ikiwemo;
Magodoro-100 ,Mashuka -50,Mablangeti -50,Vikoa 500,Madila 520 na vifaa mbalimbali kama vinavyoonekana Kwa kutambua kuwa uhitaji ni mkubwa na kwakuwa waathirika wakubwa kwenye maafa haya ni Wanawake na Watoto UWT tumewaelekeza wabunge wanawake wa CCM waendelea kuchangia kwa UWT ili tuendelee kuongeza vifaa hivi na tunatoa wito wa Wanawake wote kuguswa na kilichotokea Hanang ili waungane na UWT na tumuunge mkono Rais wetu Dkt Samia kwa kuwasaidia wananchi wenzetu wa Hanang walikumbwa na maafa.
Pia nawakaribisha wadau mbalimbali wenye nguo na vifaa vingine ambavyo vinaweza kuwa sadaka yako kwa wananchi wenzetu wa hanang, tunawakaribisha sana mziwasilishe kwenye ofisi zetu za UWT Makao Makuu Dodoma,Ofisi ndogo Dar Es Salaam zilizopo ofisi za CCM Mkoa wa Dar Es salaam.
Post A Comment: