Na Mwandishi Wetu
Maonesho haya ambayo yanajumuisha Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yanafanyika kimkakati Ili kusherehekea maadhisho ya miaka 50 ya Balaza la Mitihani na pia kuzikutanisha Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ili kutoa Elimu kwa pamoja juu ya kazi zinazofanywa na Taasisi hizo na manufaa yake kwa taifa
TAEC imeendelea kutumia fursa za namna hii katika kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya kazi inazozifanya katika nyanja za udhibiti wa Matumizi Salama ya Mionzi na uhamasishaji wa Matumizi Salama ya teknolojia ya nyuklia huku lengo kuu likiwa ni kuendelea kupanua wigo wa utoaji Elimu na kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu na faida ya teknolojia ya nyuklia katika kukuza uchumi kupitia sekta za Afya, Kilimo, Mifugo, Maji, Nishati, Ujenzi, Viwanda, Migodi na Utafiti.
Katika kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakati TAEC inatumia mifumo ya kieletroniki ambapo vibali vya mionzi hutolewa kati ya saa moja mpaka masaa matatu, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kibali kilikuwa kikichukua siku Saba
TAEC pia imeendelea kusogeza huduma kwa wananchi ambapo mpaka sasa ina jumla ya Ofisi 62 nchi nzima na kati ya hizo ofisi za Kanda ni 7, Kanda ya Kati (Dodoma na Makao Makuu), Kanda ya Mashariki ( Dar es Salaam), Zanzibar, Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya nyanda za Juu kusini, na Kanda ya Kusini
Post A Comment: