Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametangaza rasmi kushuka kwa gharama za upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi ambazo zimeridhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Silaa ametangaza hayo kwenye uzinduzi wa kliniki ya ardhi katika kata ya Chanika iliyopo halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam ambapo wananchi mbali mbali wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo la siku 25 lililoanza tarehe 16 Desemba 2023.
Amesema Mhe. Rais ameridhia kushuka kwa gharama hizo ili kuwapunguzia mzigo wa gharama za upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi na kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi kwa urahisi.
Post A Comment: