Na WAF – Morogoro
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kutoa vitendanishi vya kijipima VVU ili kuwezesha wanachi kupata wepesi pindi wanapohitaji kujua hali zao za kiafya hasa hali ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Waziri Ummy amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yenye Kaulimbiu isemayo “Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI” yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro, Disemba 1, 2023.
Waziri Ummy amesema kwa mwaka 2023 tayari wizara ya afya imeshatoa vipimo vya wananchi kujipima wenyewe vipatavyo 1,012,000 huku asilimia 89% ya waliochukua vipimo hivyo waliweza kurudisha majibu.
“Mwaka jana tulitoa vipimo 735,900 na asilimia takribani tisini waliweza kurudisha majibu ya vipimo hivyo, Tukuhakikishie Mhe. Waziri Mkuu tutaongeza idadi ya vipimo ili kuwezesha watu kujipima wenyewe ili kuweza kuondoa unyanyapaa pia kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini”. Amesema waziri Ummy.
Waziri Ummy pia amebainisha sababu ya sekta ya afya nchini kujumuisha magonjwa na mapambando dhidi ya UKIMWI pamoja na masula ya magonjwa ya ngono na homa ya ini.
“Tumeona takwimu za shirika la afya Duniani zinaonyesha kwamba kuna kushabihiana katika njia za maambukizi, udhibiti na tiba kati ya masuala ya ukimwi, magonjwa ya ngono na homa ya ini, kwa sababu hiyo tarehe 24 Novemba uliokuwa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI yaani National AIDS Control Program (NACP) umeongezewa majukumu ya kuratibu na kusimamia huduma za magonjwa ya kuambukizwa kwa njia ya ngono na homa ya ini.
Hivyo, mpango huo kwa sasa, unatambulika rasmi kama National AIDS, STIs and Hepatitis Control Program (NASHCoP)” amesema Waziri Ummy.
Post A Comment: