Loy Thomas Sabaya ameshinda kwa kishindo nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha Loy Sabaya ameshinda kwa kupata kura 463 kati ya kura 907 zilizopigwa katika nafasi ya Mwenyekiti.
Uchaguzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa Arusha International Conference Centre AICC ambapo kwa upande wa wapinzani wa Mwenyekiti huyo ambaye ni Dkt Daniel Mrisho Pallangyo aliyepata kura 374 ,Ndugu Solomoni Olesendeka Kivuyo aliyepata kura 59,Ndugu Edna Israel Kivuyo aliyepata kura 10 huku kura 1 ikiwa imeharibika.
Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye ni Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe amepongeza namna ambayo zoezi hilo la uchaguzi lilivyofanyika kwani lilikuwa la utulivu, amani kubwa kutokana hakukuwa na dalili zozote zenye kupelekea vurugu au vitendo vya rushwa
Post A Comment: