Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony John Mtaka, akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mkoa wa Arusha, muda mfupi kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, mkutano unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) leo 04.12.2023.
Msimamizi huyo wa Uchaguzo, amewataka wajumbe wote kushiriki uchaguzi huo, kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratimu kwa kuzingati maslahi mapana ya Vhama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha na Taifa.
Amewasisitiza wajumbe hao, kupiga kura huku wakizingatia, unyeti wa Nafasi hiyo ya Mwenyekiti huku akiweka wazi kutoa nafasi sawa kwa kila mjumbe kuzungumza na kujinadi na kuruhusu wajumbe kuuliza maswali ya msingi na kutokuruhusu maswali ya kejeli yanayoweza kumdhalilisha utu wa mtu.
Aidha, amewakumbusha, wajumbe, kupiga kura kwa kuwela mbele heshima kwa Chama cha ccm, na kutumia muda mfupi kukamilisha uchagzui huo.
Post A Comment: