Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Nurdin Babu ameongoza Harambee ya kuchangia mwendelezo wa ujenzi wa ofisi za konferensi Waadventista wasabato kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mkoani kilimanjaro wilaya ya Same
Zoezi hilo limefanyika tarehe 17Disemba, 2023 aliposhiriki Katika kuchangia Ujenzi huo, Mkuu wa Mkoa Nurdin Babu amechangia kiasi cha Tsh Milioni 5 kwa ajiri ya ujenzi wa ofisi hiyo
Pia RC Babu ameongoza zoezi la Harambee ambapo amewezesha kupatikana kwa fedha Tsh taslimu Tsh Milion 126,572,049,00 na Ahadi za Jumla ya Tsh Milioni 103,875,140,00 na kuwata wadau Mbalimbali kuendelea kuchangia na kufikia malengo Katika ujenzi wa ofisi za konferensi Waadventista wasabato Makao Makuu
Aidha, ametoa salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waumini na viongoz wa dini ya ya Waadventista wasabato ambapo amesema *Kipekee napenda kuwapa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amenituma niwaambie kuwa anawapenda, anawathamini na kuendelea kuwatumikia kuhakikisha huduma za kimaendeleo zinaendelea kufukishwa na Serikali anayoiongoza ya awamu ya sita na kuwataka nanyi muendelee kuwa na Imani naye.
Pamoja na hayo yote Askofu Mkuu wa Waadventista wasabato kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mkoani kilimanjaro Mussa Mzumbi Amesema Harambee ya ujenzi wa ofisi za konferensi ni kwa yoyote atakayekuswa kuchangia kwa sababu pia ni ibada kwa Mungu na kujenga mahusiano mazuri na watanzania na ambao siyo watanzania
Aliendelea kusema mradi huu ulipoanza hadi kufikia hatua hii zimetumika Milion 416,484,000. Katika changizo hili la kuchangia zaidi ya Milion 685 ni kwa ajili ya kuendeleza Mradi huu kwa kukamilisha eneo la Chin la jengo na kupandisha nguzo za Ghorofa ya kwanza na kupaua alisema Askofu Mussa Mzumbi
Aidha Askofu Mussa Mzumbi Amesema. Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama nisipo washukuru viongozi wa Serikali. Na wadini pia waumini wa kanisani la Waadventista wasabato wadau wote walijitokeza kwenye Harambee hiyo ambayo hilipewa jina la Big Day lenye lengo la kukamilisha jengo la ofisi za konferensi Waadventista wasabato kaskazini Mashariki Mkoani kilimanjaro
Askof wa kanisa la Waadventista wasabato kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mussa Mzumbi akisoma taharifa za ujenzi wa ofisi za konferensi Waadventista wasabato kaskazini Mashariki mwa Tanzania mbele Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa kilimanjaro Nurdin Babu pamoja na.waumin wote
Picha Mbalimbali ambazo Mkuu wa Mkoa kilimanjaro Nurdin Babu akiambata na Askofu Mussa Mzumbi Katika kukagua ujenzi wa ofisi za konferensi Waadventista ambazo zinajegwa kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mkoani kilimanjaro
Post A Comment: