MHESHIMIWA Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka washiriki wa kongamano Pili la Wanawake katika Biashara ndani ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kujadili namna ya kuwezesha ushiriki imara wa wanawake katika biashara ndani ya bara la Afrika.

“Ni muhimu sana katika kongamano hili mkaja na mipango mahsusi ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuwa na ushiriki wenye tija kwa wanawake katika biashara unakamilishwa”

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumatano, Desemba 6, 2023) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia  katika ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kufanyika kwa Kongamano hili kwa mara ya pili ni ishara tosha ya kuonyesha dhamira ya Nchi Washiriki wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kukuza ushiriki wa wanawake katika biashara chini ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.

“Kufanyika kwa Makongamano haya kunatoa nafasi muhimu kwa wadau mbalimbali wa kuwawezesha wanawake kujadiliana na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazokwamisha jitihada za wanawake katika biashara”

Share To:

Post A Comment: