Mkuu wa Mkoa Njombe Antony Mtaka kuunda tume itakayotatua mgogoro wa ardhi wa Wakulima na Wafugaji wa kijiji cha Kifanya kilichopo halmashauri ya mji Njombe uliodumu kwa zaidi miaka 14.
Tume hiyo itakutana na wananchi wa kijiji hicho Januari 8, 2024.“Ofisi ya Mkoa imesilikiza hoja za pande zote mbili na kubaini kuwa bado kuna mvutano hivyo naenda kuunda tume ya watu watatu watakao enda kutatua mgogoro huo kwenye sehemu iliyo tengwa kwa ajili ya wafugaji na wakulima na kujiridhisha kwa viongozi wa kijiji” ameongeza Anthony Mtaka.
Katika mgogoro kuna pande mbili za wananchi ambapo upande mmoja wanadai serikali iligawa kipande cha ardhi kutoka kwa wakulima kwenda kwa wafugaji na kusabisha wakulima kukosa eneo la kuzalisha mazao.
Mpaka sasa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 7600 linatumika kwa malisho ya mifugo katika kijiji hicho huku wakulima wakiomba kurudishiwa ardhi hiyo.
Mtaka amesema hayo Disemba 19,2023 wakati wa ziara ya kikazi katika kijiji cha Kifanya na kuagiza baraza la ardhi kupitia mikataba iliyo andikwa wakati wa makubaliano ya ugawaji eneo hilo.
Post A Comment: