Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Injinia Juma Hamsini  kutoyumbishwa na mikataba mibovu inayoingia na wajenzi ambayo inaigharimu serikali.

Mongella ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa stendi mpya eneo la Themi iliyopo kata ya Themi.

Ameagiza mchoro wa stendi hiyo uboreshwe upya ikiwemo msingi wa vibanda vitakavyojengwa hapo uwe wa ghorofa ili iwe ya kisasa zaidi na kuwaya mfano ikiwemo kutengwa eneo maalum la kupandwa miti.

“Mkurugenzi unayumba ,kwanini mnaweweseka tu kila kitu mnacho hamtaki kumaliza mgogoro ule wa stendi ndogo,sisi viongozi tumewekwa hapa Kwa maslahi mapana ya wanaarusha na si maslahi ya wanasiasa,hatujengi nchi kwa kumwangalia mtu,tusijizimishe data au kujitoa ufahamu sisi wengine hatupo kwenye mihemko hiyo” alisema.

Naye Mkurugenzi wa jiji hilo, Hamsini amesema halmashauri hiyo inajenga stendi hiyo mpya ili kupunguza msongamano wa daladala zinazopaki kando kando ya barabara kuu eneo la Kilombero na stendi ndogo lakini alisisitiza mfumo mpya wa Tausi ndio utaondoa changamoto ya mgogoro wa stendi ndogo unaofukuta na kuagiza kuchukua hatua zaidi katika jambo hilo la mgogoro wa stendi ndogo.


H.T ; HabariLeo

Share To:

Post A Comment: