Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Mohamed Mchengerwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuandaa mpango wa kitaifa wa kuhakikisha  barabara za vijijini na mijini zinapitika kwa asilimia 85 ifikapo 2025.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo leo katika Kijiji cha Mohoro alipohudhuria na kushuhudia hafla ya utiaji saini pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Bibi Titi Mohamed litakalogharimu Sh.Bilioni 11.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kilitoa ahadi ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami na teknolojia mbadala kwa asilimia 85 hivyo utekelezaji huo unatakiwa kufanyika kwa maeneo ambayo bado hayajafikiwa.

"Mpango huu unifikie mara moja bila kujali gharama ni sh. ngapi nileteeni nikishapata tunajipanga sasa kwenda kutafuta fedha kumuomba Mh. Rais atupatie fedha ujenzi wa barabara zote nchi nzima katika mikoa yote 26 na wilaya zote maana yake ni kuwa Mhe. Rais na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 inatutaka kujenga barabara zote kwa kiwango kizuri, ifikapo 2025 tufikie asilimia 85 tutafanya maamuzi zipi tuzianze,"amesema.

Akizungumzia umuhimu wa daraja la Bibi Titi, Mhe. Mchengerwa amesema litakwenda kuondoa vifo vya wananchi vilivyokuwa vikitokea kipindi cha mvua wakati wananchi wakivuka katika daraja la awali.

Vilevile ameeleza kwamba kilio cha ujenzi wa daraja hilo ni cha muda mrefu na sasa wakazi wa vijiji vya Mohoro na Chumbi ambavyo kuna wakazi zaidi ya 60,000 hali zao za kiuchumi zitakwenda kuimarika na 

kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na Wataalamu wa TARURA Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Rufiji kusimamia kwa weledi mradi huo. 

Share To:

Post A Comment: