Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi wa chama Cha mapinduzi CCM taifa , Amewataka viongozi na wanachama kuacha kutengenezea ajali kazini.
Hayo yamejiri katika ziara ya Katibu mkuu Wazazi Taifa ndugu Gilbert Kalima Katika kata ya Esilalei Wilayani Monduli alipofanya ziara ya kukagua Uhai wa Jumuiya na Chama kwa ujumla, Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi ikiwemo miradi ya jumuiya ya wazazi inayotekelezwa Wilayani humo,ikiwemo mashine ya kukoboa na kusaga yenye Thamani ya shilingi Millioni 11.
Ndugu Gilbert Kalima pamoja na kusisitiza Umoja na Mshikano katika uongozi amempongeza Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya Ndugu Kisioki Moitiko kwa kuendelea kuinua jumuiya hiyo ya wazazi kiuchumi, na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano na utendaji wa Kiongozi huyo.
"Hapa Emesema bila uchumi mambo hayaendi au sio, na ni kweli siku hizi siasa ni uchumi ,bila uchumi huwezi kufanya siasa, bila uchumi wa jumuiya ninyi ngazi ya wilaya ya monduli hamuwezi kufanya ziara katika kata zote 20 ,hamuwezi kufanya ziara kwenye vijiji na vitongoji vyake vyote hivyo ambavyo pia mwenyekiti wa halmashauri alivisema hapa, kwa hiyo bila uchumi haya yote hayawezekani na katika hili nikupongeze mwenyekiti kwa majitoleo Yako, lakini nikupongeze kwa tamaa yako kwa sababu umesema nia yenu kama wilaya ni kuhakikisha Kila kata inapata mradi wake, Tuacheni siasa za migongano za kuvunjiana heshima ,Leo kwa mfano tumemchagua kiongozi ,Mfano mwenyekiti hapa akifanya KAZI Kwa juhudu kelele zinaanza anataka nafasi flani (ubunge), kama tuliamua kumchagua tumuache Kwa nafasi yake amalize matakwa ya kile alichokiomba tutampima kwa KAZI zake , viongozi tuache kudhalilishana unamkuta kiongozi labda wa chama anamuarisha wa serikali wee Fulani fanya hivi mara wee nani nakupa siku kadhaa tatua hikiii noooo humdhalilishi huyo mtu unaidhalilisha CCM" alisema ndugu Kalima
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Ndugu kisioki Moitiko Amesema KIU yake kubwa katika uongozi wake ni UCHUMI kwa jumuiya hiyo , huku mfano tayari ushaonekana baada TU ya kuzinduliwa Kwa mashine ya kusaga na kukoboa yenye thamani ya shilingi millioni 11, na kusem mikakati yake kubwa ni kuhakikisha Kila kata inakuwa na mradi wake ili kuwasaidia viongozi kufika katika vikao mbalimbali pindi tu watakapohitajika pamoja na ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa jumuiya hiyo ,inayotaaajiwa harambee yake kufanyika February 2024 bila uchumi siasa haiendi.
Aidha kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi wilayani humo Bi Rukia Mbasha ,Amemuhakikishia katibu mkuu jumuiya ya wazazi ushindi kwa Uchaguzi wa serikali za mitaaa kwa mwaka 2024 , na kusema hii ni kutokana kuwa Chama, jumuiya na viongozi wengine kuwa wamoja katika majukumu.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Wilayani Monduli , Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh Issack Kadogoo , Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwani bajeti kwa mwaka wa Halmshauri ya wilaya hiyo imependa Kwa Kasi
" Mh katibu mkuu naomba nikupe takwimu kidogo wakatia Rais Samia anaingia madarakani halmashauri ya monduli tukuwa bajeti yetu kwa mwaa ni billioni 31, alipoingia madarakani mwaka wa kwanza bajeti yetu ikapanda Hadi billioni 42, yenye mchanganuo ufuatao ,mishahara ya watumishi billioni 22, miradi ya maendeleo billioni 20 yenye mchanganuo ufuatao fedha kwa ajili ya chakula mashuleni billioni 6 kwa mwaka tunapata kwa halmashauri ya Monduli ,miradi ya maji tunapata billioni 8,miradi ya Barabara billioni 2 miradi mingine ikiwemo afya usiseme hakika Rais Samia kaitendea haki Monduli ." Amesema issack
Post A Comment: