Na John Walter-Manyara
Mahakama ya wilaya ya Babati imefuta shauri la jinai lililofunguliwa na wakili Peter Madeleka dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul la kumfanyia shambulio la mwili Hashim Ali.
Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 27,2023 na Hakimu Mkazi wilaya ya Babati Victor Kimario baada ya mwendesha mashtaka wa serikali kuona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo na ameiondoa kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) Cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Nje ya mahakama wakili upande wa mlalamikaji Peter Madeleka amesema wanakusudia kukata rufaa kwa kuwa hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama.
Madeleka akiwa na mawakili wengine Thadei Lister na Peter Masanja walifungua kesi dhidi ya Mbunge Paulina Gekul wakidai alimfanyia kitendo hicho Hashim Ali kwa kumuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.
Upande wa mshtakiwa uliwakilishwa na wakili Ephraim Kisanga.
Post A Comment: