Na John Walter-Manyara
Idadi ya Watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, Wilayani Hanang imeongezeka na kufikia 63 baada ya kupatikana miili zaidi wakati wa zoezi la uokoaji likiendelea.
Taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo wakati wa ibada maalum ya kuaga miili hiyo, imeeleza kuwa kati ya marehemu hao, wanaume ni 23 na wanawake ni 40 na kwamba kati ya marehemu wote, watu wazima ni 40 na watoto chini ya miaka 18 wapo 23.
Kati ya waliofariki, wenye Miaka 18 na zaidi ni Wanaume 14 na Wanawake 26, wenye chini ya Miaka 18, Wanaume ni 9 na Wanawake 14.
Aidha, majeruhi katika maoporomoko hayo ni 116, kati yao wanaume ni 56, Wanawake ni 60.
Majeruhi watu wazima ni 60 na wanume 26 na Wanawake 31 ,watoto chini ya miaka 18 ni 66 ambapo kati yao 66 wanaume ni 27 na Wanawake 29.
Waziri mkuu amesema serikali inagharamia Shughuli zote za mazishi, kuhudumia Majeruhi na kutoa malazi na chakula kwa wasio na makazi.
Post A Comment: