Na John Walter-Manyara
Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya maji kutoka mlima Hanang'imeongezeka na kufikia 49.
Taarifa ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga imeeleza kuwa miili ya watu wawili imeopolewa kutoka kwenye Matope na kuongeza idadi kutoka 47.
Sendiga amesema Mawaziri na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na Wataalamu wanaendelea kuwasili wilayani Hanang'.
Amesema zoezi la kutafuta miili Mingine linaendelea likiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Amesema huenda vifo zaidi vikaongezeka kwa kuwa bado watu wanadai kuwa hawawaoni ndugu zao tangu tukio hilo litokee Jana Jumapili Desemba 3,2023.
Post A Comment: