Na John Walter-Manyara
Serikali imesema jumla ya idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali kutokana mafuriko na maporomoko ya maji Katesh na Gendabi wilayani Hanang' Mkoani Manyara imefika 93.
Awali mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga alitangaza kuwa Majeruhi walikuwa ni 85 hadi Jana jioni.
Mganga mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema majeruhi 11 waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara, watano ni Watoto ambapo wawili wapo kwenye uangalizi maalum, wawili wamefanyiwa upasuaji wa kuondolewa bandama kutokana na majeraha waliyoyapata, watatu watatu wamefanyiwa upasuaji Mdogo wa mifupa na kuwekwa mifupa vizuri kwa kuwa walipata mvunjiko.
Serikali imewaongezea nguvu Madaktari Hospitali ya rufaa mkoa wa Manyara kwa kuwapatia Madaktari 10 kutoka hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na wengine 12 wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha na Singida.
Katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt.John Jingu amesema tangu janga lililotokea Desemba 3,2023, wizara imeendelea kujipanga kuwahudumia kikamilifu majeruhi wote.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kila kitu kinakwenda sawa kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan.
Post A Comment: