Na John Walter-Manyara
Serikali imesema hakuna uhaba wa Sukari nchini na kwamba upungufu uliopo hivi Sasa kwa mikoa ya kaskazini unatokana kiwanda cha TPC cha Moshi mkoani Kiilimanjaro kupunguza uzalishaji na Manyara Sugar cha mkoani Manyara kusitisha uzalishaji kutokanana ukosefu wa mali ghafi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Manyara Sugar kilichopo kijiji cha Matufa Wilayani Babati ambacho kimesitisha uzalishaji kutokanana ukosefu wa mali ghafi.
Kauli hiyo ya Waziri Kijaji inakuja wakati huu ambapo Sukari imeadimika mitaani ambapo kilo moja ya Sukari iliyokuwa inauzwa shilingi 3,200 kwa rejareja katika miji ya Babati na Karatu Sasa inauzwa kati ya shilingi 3,800 hadi 4000, hali ambayo Wananchi wanaomba Serikali ifuatilie na kutafuta ufumbuzi.
Afisa uhusiano Kiwanda cha Manyara Sugar John Jeu amesema wamesitisha uzalishaji kwa sababu ya ukosefu wa malighafi za kutengenezea sukari.
Afisa uhusiano Kiwanda cha Manyara Sugar John Jeu amesema wamesitisha uzalishaji kwa sababu ya ukosefu wa malighafi za kutengenezea sukari.
Amesema kwa sasa serikali inaangalia utaratibu wa kusambaza sukari kutoka mikoa ambayo kuna hodhi kubwa kwenda mikoa yenye upungufu ili kukabiliana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo, huku akitoa wito kuwataka wakulima kuchangamkia fursa ya kilimo cha miwa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Sukari nchini.
Amesema kwa sasa serikali inaangalia utaratibu wa kusambaza sukari kutoka mikoa ambayo kuna hodhi kubwa kwenda mikoa yenye upungufu ili kukabiliana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo Kwa sasa Viongozi ngazi zote kuhamasisha kilimo cha miwa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa sukari na bei kupanda.
Hata hivyo ameshauri uwepo wa mpango wa muda mrefu ukiwemo uchimbaji wa mabwawa makubwa yatakayosaidia kuhifadhi maji kwa ajili ya umwagiliaji ili kuwaondolea wakulima wa miwa utegemezi wa msimu wa mvua pekee.
Amesema serikali imeandaa Mpango wa visima Zaidi ya 680 ambapo 150 vitachimbwa katika Wilaya ya Babati na ameelekeza 30 vichimwa katika mashamba ya miwa ya Magugu.
Mfafanyabiashara Peter Mallya wa Mjini Babati amesema kwa sasa wanapata sukari kwa tabu kutokana na kiwanda cha TPC alikokuwa anachukulia kupunguza Uzalishaji.
Amesema kwa sasa mfuko kilo moja ya sukari iliyokuwa inauzwa shilingi 3000 imepanda hadi shilingi 4,000.
Post A Comment: