NA DENIS CHAMBI,  TANGA.

CHAMA cha Mapinduzi 'CCM' kimetoa onyo kali kwa wanachama wake wakiwemo madiwani na wabunge ambao wameshaanza kujitengenezea mazingira ya kupata kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 huku kikiwashukia wenyeviti wa mitaa vijiji na vitongoji ambao wameshindwa kufanya mikutano kikisema kuwa hakitakuwa tayari kumbeba yeyote ambaye hakuwajibika ipasavyo.

Msimamo huo wa chama ulitolewa na katibu wa siasa na uenezi  organize seesheni Taifa na mjumbe wa halmashauti kuu Issa Gavu  december 7, 2023 wakati akiwa kwenye mkutano wa baraza la wazee wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga ambapo amesema kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika 2024 na hata ule uchaguzi mkuu wa 2025  mgombe yeyote yule atapimwa kulingana na alichokifanya utayari wake wa kuwatumikia wananchi na kutatua kero na sio kuwa tegemezi ndani ya chama.

"Ninajua wapo baadhi ya wabunge na madiwani wanahangaika kupanga safu  kwa wenyeviti wa vijji vitongoji na mitaa  kwaajili ya kujitengenezea urahisi kwenye safari yao ya 2025 kwenye uchaguzi mkuu   nikuombe uwe mwenyekiti,  diwani au mbunge kama jimbo  lako tutapoteza vijiji,  vitongoji au  mtaa   ujitafakari wewe mwenyewe hatutakuwa na muda wa kumbembeleza kiongozi wala hatotokuwa tayari kumbeba mtu , makundi yametuumiza kwa muda mrefu ndani ya chama chetu  hatuna nafasi ya kubeba mtu kwa sababu ya nasaba au urafiki au kwaajili ya kutengeneza makundi ndani ya chama chetu" alisema Gavu.

"Wapo baadhi ya viongozi hasa wenyeviti  wa mitaa vitongoji wameshindwa kufanya mikutano ya kusoma mapato na matumizi au mikutano ya kawaida nawahakikishieni kama kuna mwenyekiti ambaye hayuko tayari kusimama na kusimamia kanuni na maelekezo ya serikali katika kutimiza wajibu wake mwenyekiti huyo kwenye chama chetu hana nafasi tunahitaji kuwa na wenyeviti watakao kuwa tayari kwenda kujitoa na kujituma kwenye changamoto za watu na kuzipatia  ufumbuzi"  alisisitiza.

Awali akizungumza mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman  aliielekeza serikali ya mkoa wa huo kuhakikisha inaweka utaratibu mzuri kwa wazee kupatiwa huduma za afya katika vituo vya afya zahanati na hospitali hii ikiwa ni madai ya wazee hao walioeleza kuwa wamekuwa wakipata changamoto pindi wanapofika kupata huduma.

"Haiwezekani kwamba kila kiongozi anayekuja  lazima wazee walalamike kuhusu suala la afya mimi kama kiongozi mwenye dhamana ndani ya mkoa huu  nasema sasa ifike mwisho haiwezekani wazee hawa ambao tumekuta chama katika mikono yao wameipigania mpaka serikali yetu  halafu wanaendelea kupata tabu hivyo kuwathamini kwao ni kule kutekeleza yale ambayo tunapaswa kuyatekeleza" alisema Abdurlahman.

Akizungumzia mikopo ya asilimia 10 ya mapato  ya halmashauri amabayo itaanza kutolewa rasmi baada ya serikali kuisitisha kutokana na uwepo wa vikundi hewa  na kutafuta utaratibu mpya  mwenyekiti huyo amewaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha vikundi vyote vitakayopewa mikopo hiyo vinasajiliwa na kufuata taratibu zote mpya zilizowekwa na serikali.

"Ipo changamoto ambayo kila mahali unapoenda unaikuta ya asilimia 10 ya mapato halmashauri ambayo haina riba nitoe wito kwa wakurugenzi wote kuhakikisha tunatoa mikopo kwa vikundi vya akina mama,  walemavu na vijana vilivyosajiliwa na sii vikundi hewa kama ilivyokuwa hapo awali ili vikundi hivi viweze kujiendeleza kiuchumi" aliongeza.

Mkuu wa mkoa wa Tanga ambaye pia ni kamisaa wa chama cha mapinduzi Waziri Kindamba amebainisha kuwa ndoto ya serikali katika kuwekea mazingira rafiki ya kiuchumi katika mkoa huo  bado inaishi ambapo hivi karibuni  amepatikana mwekezaji kutoka nchini Spain  ambaye anatarajiwa kuja kujenga kiwanda cha kuchakata  samaki.

"Hivi karibuni tulienda  nchini  Spain kwaajili ya kuleta mwekezaji mkubwa kwaajili ya kujenga kiwanda cha kuchakata samaki katika mkoa wa Tanga ni matarajio yetu kiwanda hicho kikamilike kabla ya mwaka 2025  mchakato wa uanzishwaji wa kiwanda hicho umeshaanza  na sasa tupo katika michakato mbalimbali ya upembezi yakinifu wa kimazingira" alisema Kindamba.
 
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi  'CCM' mkoa wa Tanga akizungumza katika mkutasno huo uliofanyika ukumbi wa Simba Mtoto jijini hapa
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa chama cha mapinduzi mkopa wa Tanga akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba  ambaye pia ni kamisaa wa Chama cha mapinduzi akitoa salamu za serikali katika mkutano huo

Baadhi ya wazee wa kutoka katika wilaya nane na halmashauri 11 za mkoa wa Tanga wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha mapinduzi 'CCM'
Mwenyekiti wa baraza la wazee mkoa wa Tanga mzee Mnyamisi(kulia) akimlaki katibu wa NECorganizesheni mara baada ya kuwasili mkoani Tanga December 7,2023.
Share To:

Post A Comment: