Na John Walter
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametaka Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kufanya uhakiki mapema katika maeneo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa huruma yake amewapa wananchi.
Waziri Silaa ameyasema hayo jijini Mwanza wakati akipokea malalamiko ya wakazi wa jiji hilo ambapo mmoja wa wakazi hao Bi. Gift William alimfikishia malalamiko ya eneo lake ambalo lina mgogoro na shule.
Amesema maeneo mengi ambayo wananchi wamevamia lakini Serikali imeamua kuwapa kwa huruma, yamekuwa hayafanyiwi uhakiki mapema jambo ambalo linafanya wavamizi hao kuweka makazi ya kudumu na kupelekea kuzalisha mgogoro.
Post A Comment: