Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imefanikiwa kujenga MFUMO unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus(GovESB).
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mafanikio ya mfumo huu ambao pia lilikuwa ni agizo la Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Mamlaka imefanikiwa kujenga Mfumo unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa, ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus (GovESB) mfumo umetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kuzingatia kifungu cha 48 (2)cha Sheria ya Serikali Mtandao Na 10 ya mwaka 2019,kinachoitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao kuanzisha na kuendesha mfumo unaoweza mifumo ya TEHAMA Serikalini kuwasiliana na kubadilishana taarifa".
"Sambamba na kutekeleza matakwa hayo ya kisheria,pia Ujenzi wa mfumo wa GovESB ni utekelezaji wa agizo la Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,la kuhakikisha mifumo ya TEHAMA katika Taasisi za Umma inaunganishwa na kubadilishana taarifa".
Pia Mhandisi Ndomba ameeleza lengo la mfumo huu ambapo amesema ni kuziwezesha Taasisi za Umma kubadilishana taarifa kidijitali kwa usalama kupunguza urudufu wa mifumo,kuongeza ufanisi wa utendaji Kazi pamoja na kuomoa muda.
"Mfumo wa ubadilishanaji taarifa Serikalini GovESB ni mfumo wa kielekroniki unaounganisha mifumo ya TEHAMA ya Taasisi za Umma iweze kusomana na kubadilishana taarifa kila inapohitajika. Lengo la mfumo huu ni kuziwezesha Taasisi za Umma kubadilishana taarifa kidijitali kwa usalama, kupunguza urudufu wa mifumo, kuongeza ufanisi wa utendaji Kazi, kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kuokoa muda kwakuwa taarifa hupatikana kwa wakati".
Aidha amezungumzia changamoto za awali kabla ya mfumo huu nakueleza kuwa awali ili mifumo ya TEHAMA iweze kusomana ililazimika kuunganisha mfumo Mmoja kuzungumza na mifumo mingine kila inapohitajika.
"Hapo awali ili mifumo ya TEHAMA iweze kusomana, ililazimika kuunganisha mfumo Mmoja kuzungumza na mifumo mingine kila inapohitajika yani "point-to-point connections" uunganishwaji huuulisababisha urudufu wa mifumo,kupungua kwa usalama, kupunguza ufanisiwa mifumo kuongeza gharamza Usimamizi na uendeshaji wa mifumo ya TEHAMA".
Pia Mamlaka hii ya Serikali Mtandao imeshirikiana na taasisi nyingine za Umma ikiwemo TRA, TPA na Wizara ya Fedha katika kusanifu mfumo wa pamoja wa kielekroniki wa uondoshaji wa shehena maeneo ya forodha(Tanzania Electronic Single Window System - TeSWS).
"e-GA imeshirikiana na Taasisi nyingine za Umma ikiwemo TRA, TPA, na Wizara ya Fedha katika kusanifu mfumo wa pamoja wa kielekroniki wa uondoshaji shehena maeneo ya forodha, mfumo huu ni moja ya miradi inayotekelezwa chini mradi mkubwa wa kujenga uwezo wa kitaasisi wa kukusanya mapato ya ndani na Usimamizi wa Mali Asilia( Institution Support Project On Domestic Resources Mobilisation and Natural Resources Governance- ISP-DRM-NRG), unasimamiwa na Wizara ya Nishati".
Mfumo huu ulianza kufanya Kazi kama majaribio mwaka 2022 na mwaka 2023 January mfumo huu wa GovESB ulinza kufanya Kazi zake Rasmi na Hadi Sasa Taasisi jumala ya 109za Umma zimeunganishwa katika mfumo huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao ( e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba wakati alozungumza na wanahabari kuhusu mafanikio ya mfumo huo Leo Jijini Dodoma
Post A Comment: