Na.Ashura Mohamed - Arusha 

Benki ya CRDB imemkabidhi gari aina ya Toyota Vanguard kwa mshindi wa jumla wa kampeni ya benki ni simu banking  lenye thamani  ya zaidi ya milioni 40, mkoani  Arusha.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari hilo katika ofisi za benki hiyo zilizopo USA River wilayani Arumeru Dkt. Bakari George ambaye pia ni mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru ameeleza siri ya ushindi wake kuwa ni matumizi ya asilimia 95 ya simu banking.

"Mara baada ya kutangazwa mshindi nimempigiwa siku nyingi sana za kutaka kujua nimefanya nini ila Mimi Siri kubwa nimekuwa nikitumia simu yangu kufanya miamala mbali mbali,nalipa ada,nanunua vocha,nanunua umeme,nalipa maji yaani kifupi Kila kitu natumia simu yangu kufanya Malipo ndio Siri ya Mafanikio na nimeanza zamani Sana sio Sasa"Alisema dkt.Bakari

Aidha alisema kuwa katika Ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia huduma ya simu banking haikwepeki na inaokoa rasilimali fedha,muda na inampatia mteja uhakika wa muamala pamoja na kumpatia ristiti papo kwa hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi CRDB,bw.Stephen Adili alisema katika kampeni yao wametoa magari 6 ambapo matano kati yake ni  Toyota Crown na Van Guard moja lililohitimisha kampeni hiyo na  kumpata mshindi wa jumla ambaye pia amepata gari.

Bw.Adili alitumia fursa hiyo kumshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kutengeneza miundo mbinu bora ya biashara na kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira wezeshi hali  inayopelekea benki hiyo kurudisha faida kwa wateja.

"Kwa sasa kuna mazingira mazuri sana ya kufanya biashara ambapo benki yetu inaendelea kukua siku hadi siku ambapo hatua hii inapelekea kuchechemua uchumi,na kuwezesha wateja wetu kukopa mikopo mikubwa na kufungua biashara ambazo zinaongeza ajira na kuongeza faida kwa watu."Alisisitiza bw.Adili

Alisema kuwa benki hiyo kiongozi hapa nchini itaendelea na kampeni mbali mbali ambapo zitasaidia kurudisha faida kwa Jamii na kuwezesha watanzania kunufaika na Benki hiyo bunifu hapa nchini.

Kampeni hiyo iliyokuwa inahamasisha wateja kutumia simu zao kijihidumia kifedha  ilikuwa na zawadi mbalimbali ambapo simu zaidi ya 200 zimetolewa,fedha taslimu milioni 300,na komputa mpakato kwa wanafunzi, na magari 6.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa pamoja na mshindi wa Jumla wa gari aina ya Vanguard katika picha ya pamoja katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika ofisi za benki hiyo zilizopo Usariver wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mshindi wa Jumla wa Gari aina ya Van guard dkt.Bakari George akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Benki hiyo ambao hawapo pichani wakati wa halfa ya makabidhiano ya gari hiyo.

Mkuu wa Kitengo Cha Wateja binafsi kutoka Benki ya CRDB bw.Stephen Adili akimkabidhi namba mshindi wa Jumla wa Gari aina ya Van guard  dkt .Bakari George na pembeni yake ni Meneja Kanda ya Kaskazini bw.Cosmas Sadat.

Wadau mbali mbali wakifuatilia Kwa makini hafla ya makabidhiano ya mshindi wa Jumla.


Share To:

Post A Comment: