Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kufunga mara Moja shule ya Msingi Kigulunde baada ya kubaini eneo ilikojengwa shule hiyo ni mkondo wa maji na tayari majengo yake yana Nyufa hali inayohatarisha usalama wa wanafunzi na walimu.
Shule hiyo yenye wanafunzi 49 na walimu wawili iliwahi kukumbwa na mafuriko mwaka 2011 na baadhi ya majengo kusombwa na Maji ambapo kipindi hicho iliamuliwa wanafunzi kupelekwa shule jirani ya Msingi Mtii
Katika ziara yake mkuu huyo wa wilaya aliye ambatana na wajumbe wa kamati ya usalama ameagiza shule hiyo kufungwa na wanafunzi kupelekwa shule iliyo jirani, shule ya Msingi Mtii kuendelea na masomo wakati hatua myingine zikiendelea ikiwemo uwesekano wa kujenga shule mpya eneo rafiki litakalo kuwa salama.
Viongozi wa Kijiji hicho wamebainisha kuwa eneo la shule lina ukubwa wa Hekari Saba na mkuu huyo wa wilaya akashauri endapo wakazi wa eneo hilo wanauhitaji wa shule kushirikiana na wataalam wa Halmashauri kupata eneo linalofaa na kuanza msaragambo kujitolea michango na nguvukazi kujenga maboma Kisha kuwesesha urahisi kwa serikali kumalizia kama inavyofanyika kwenye maeneo mengine.
Akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya, mdhibiti ubora wa shule amesema walisha tembelea shule hiyo mwaka 2020 wakabaini kuwepo wanafunzi wanaoe delea kutumia shule hiyo na walishatoa ushauri kwa Halmashauri kuifunga kutokana na hatari iliyopo, huku taarifa ya Halmashauri nayo inaeleza upo mpango wa ujenzi wa shule mpya kwnye eneo hilo kupitia Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 1.86 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule za Msingi (BOOST) kwa wilaya ya Same pekee, ambapo Madarasa 52 yamejengwa kwneye shule 10, matundu ya vyoo 40 na majengo 2 ya utawala.
Post A Comment: