Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda na msafara alioambata nao wamejikuta katika Simanzi nzito mara baada ya kumuona Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope ambalo lilikuwa limemuonea mwili mzima na kumsomba mita kadhaa.


Akizungumza leo alipomtembelea Mwanamke huyo katika Kituo cha Afya Gendabi mahali ambapo ndipo kulikuwa na Maafa makubwa kufuatia mafuriko yaliyotokea mara baada ya Mlima Hanang kupasuka.

"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama huyu ambaye alisombwa na tope na kuweza kuokolewa kwenye tope hilo na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua salama

Mtoto wa kiume 3/12/2023 kwa kweli nimelia uchungu baada ya kusikiliza simulizi za Mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku mjamzito wa miezi tisa hakika hakuna kama Mama . Namshukuru sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha Mama huyu kujifungua salama na mtoto yupo Salama na ameitwa Mussa ."

Aidha Mwenyekiti amesema Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea mahitaji ya kutosha

Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang .





Share To:

Post A Comment: