Na John Walter-Manyara

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha huduma ya Chakula ni ya Uhakika kwa wahanga katika maeneo yaliyoaathiriwa vibaya na maporomoko ya udongo,mawe na miti katika kata za Dumbeta, Katesh, Jorodom na Gendabi wilayani Hanang' Mkoani Manyara Desemba 3,2023.

Baadhi ya wahanga wamepongeza na kushukuru jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali  kwa kuwafanya wajisikie kuwa na amani muda wote licha ya maafa yaliyowakumba.

Aidha wamemshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuwafariji kwa kuwatembelea waathiriwa Licha ya kuwa na majukumu mengine nje ya nchi.

Saa chache baada ya Maafa kutokea Hanang', Rais Samia Suluhu Hassan akiwa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu Dubai kwenye Mkutano wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi (COP28) alituma salamu za Pole na kuagiza wizara zote za Kisekta kufika Hanang' kutoa Msaada wa haraka jambo ambalo lilitekelezwa kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa chini ya wizara ya nchi, ofisi ya Waziri Mkuu,sera,Bunge na Uratibu inayoongozwa na Waziri Jenista Mhagama,  na mpaka Sasa Shughuli zinaendelea kuyarejesha maeneo yaliyoathiriwa katika hali ya kawaida.
 
Wadau mbalimbali wanaendelea kujitokeza kutoa misaada ya kibinadamu wilayani humo zikiwemo fedha, vyakula, mavazi, mbolea na mbegu za kupanda mashambani.
Share To:

Post A Comment: