OR-TAMISEMI
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema kwa kipindi cha miaka miwili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoa huo umepokea takribani Sh.Bilioni 754 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza katika uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchuguzi ya CCM 2020-2025 ya Jimbo la Vunjo leo, amesema Mhe. Rais ameutendea haki mkoa huo na kati ya fedha hizo Sh.Bilioni 92.29 zimejenga miundombinu ya afya hususan hospitali za Wilaya, Majengo ya huduma za dharura, majengo ya wagonjwa mahututi, nyumba aa watumishi, vifaa tiba hususan ni vile vya majengo ya kufanyia upasuaji wa dharura, mionzi pamoja na ununuzi wa madawa.
Aidha, amesema Sh. Bilioni 70.3 zimetumika kujenga shule mpya za Sekondari pamoja na msingi, nyumba za walimu pamoja madarasa ya awali.
“Eneo la miundombinu kupitia Wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA) Mkoa huu umepokea Sh. Bilioni 32 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara.Maeneo mengine ambayo fedha zimetolewa ni pamoja na mikopo iliyotolewa kwenye vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, fedha za TASAF, TANROAD pamoja na fedha za kuimarisha utawala bora,”amesema.
Hata hivyo, amesema atika Jimbo la Vunjo pekee Sh.Bilioni 3.8 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Post A Comment: