Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeshiriki kwenye zoezi la kutoa msaada kwa wahanga waliokumbwa na changamoto ya mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoisababishwa na mvua kubwa kwenye kijiji cha Katesh, Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.
AICC ilikabidhi msaada wa mablanketi 200 na kiasi cha shilingi milioni 12 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga aliyeambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt Jim James Yonazi na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Karoline Mthapula.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Afisa Uhusiano Mwandamizi Bw. Fredrick Maro ali
Post A Comment: