Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ameagiza watu wanaolala katika zahanati ya Leremeta iliyopo Kata ya Sinya Wilayani Longido kuondoka mara na magodoro yao kwani eneo hilo si nyumba ya kulala wageni kwani tokea Zahanati hiyo ijengwe ni mwaka wa tatu sasa na hakijawahi kutoa huduma yoyote kwa wananchi wa eneo hilo.

Zahanati hiyo iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya milioni 88 ambapo lengo lilikuwa ni kuwasaidia wananchi wa kata hiyo ambapo kwa sasa imegeukia kuwa eneo la kulala.

Akiwa katika ziara ya kikazi Mkuu huyo wa mkoa ameagiza pia dawa zilizopo stoo katika kituo hicho ambazo hazijawahi kutumiwa na wagonjwa ziondolewe ikiwemo kusafishwa kituo hicho na kupakwa rangi upya ikiwemo uwekaji wa kingo za maji.

Rc Mongella alizungumza hayo katika eneo la Sinya baada ya kukagua mradi wa nyumba ya watumishi inayojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kwa gharama ya zaidi ya Milioni 92.

Rc Mongella alihoji inakuwaje kituo Cha afya kijengwe dawa zipelekwe eneo husika ila zimefungiwa stoo na kuisha nguvu huku wananchi wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita sita kupata huduma za afya katika Kata hiyo kutokana na ukosefu wa wahudumu.

"Sasa wewe Mganga Mkuu wa Wilaya ya Longido Mathew Najai Baki hapa kituoni kwaajili ya kutoa huduma za afya kwa wananchi hao  na hiki kituo kifanyiwe usafi hapa sio nyumba ya kulala wageni(gest house)halafu kwanini dawa zipo ila hazijawahi kutolewa kwa wananchi kwahiyo hapa hakuna mtu anaumwa,mnaleta dharau kwa wananchi,huku hakuishi watu, kwanini mlikuwa hamtaki nije huku eti mnadai kunachangamoto ya barabara ,mlikua siji eeh"

Pia  alihoji kwa Mratibu wa Tasaf,Namei Lobulu kwanini mradi wa ujenzi wa nyumba ya kuishi watumishi wawili na familia mbili wa afya  haijakamilika tangu Mei ,23 mwaka huu huku ikiwa imetumia kiasi cha sh,milioni 92,410 huku sh,milioni 75.321 zikiwa zimeshatumika.

Ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo,Marko Ng'umbi akipewa maelekezo hadi Desemba 8 ,mwaka huu nyumba hiyo ya watumishi iwe imeshakamilika kwani wananchi walichangia nguvu zao lakini hakuna huduma za afya zinazotolewa kituoni hapo.

"Hapa kuna uzembe fulani hivi sasa kasoro zilizopo hapa zirekebishwe ikiwemo kituo cha afya kisafishwe,dawa zipangwe zimavyostahiki,usafi ufanyike ili kianze kutoa huduma za afya"

Wananchi wa eneo hilo walichangia kiasi cha sh,milioni 24.420 lakini hadi sasa hakuna huduma inayotolewa kituo hapo.






Share To:

Post A Comment: