Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesema kuwa serikali inatekeleza miradi nane  yenye thamani ya sh. Bilioni 13.3 kwa ajili kutoa huduma ya maji kwenye Vijiji 22 katika Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.

Mhandisi Mahundi ameeleza  hayo leo Novemba 24, 2023, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa Wilayani Mbozi, Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Songwe.

Alisema  kuwa jumla ya vijiji 99 vimepatiwa huduma ya maji kati ya Vijiji 121 vilivyopo wilayani Mbozi.

Aliongeza kwa kusema kuwa serikali inaendelea na jitihada za   kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika miji ya Vwawa na Mlowo wilayani mbozi kupitia mradi wa  ukarabati wa chanzo cha maji Mwansyania na  upanuzi wa mtandao wa maji wenye Jumla ya thamani ya sh. bilioni 3.9.

Aidha, Mhandisi Mahundi alisema mbali na jitihada hizo, serikali ipo kwenye mchakato wa  utekelezaji wa mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Momba ambao unagharimu kiasi cha sh.  bilioni 340 kwa ajili ya kutatua kero ya maji katika miji ya Tunduma, wilayani Momba pamoja na miji ya  Vwawa na Mlowo, wilayani Mbozi.

Share To:

Post A Comment: