NCHI ya Tanzania inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano mkuu wa Kimataifa wa Usonji unaotarajiwa kuwa na wageni kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika.


Akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam Mwanzilishi wa Taasisi ya Kulea watoto wenye hali ya Usonji (VICTORIOUS CENTER OF EXCELLENCE) Sarah Laiser amesema Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi Disemba 02 na 03,2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni 1200 kutoka nchi mbalimbali.

"Mkutano huo umeandaliwa na taasisi yetu ya Victorious center ikishirikiana na ambapo tunalea na taasisi ya Kimataifa (AUTISM CONNECT) kutoka nchini India tumeweza kuandaa mkutano huu mahususi kwa lengo la kukuza uelewa kwa jamii kuhusu hali ya usonji na namna ya kuwasaidia watu wa aina hiyo kukuwa katika hali nzuri."

Aidha, amefafanua zaidi Kuongezeka kwa watu wenye changamoto ya usonji ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa huku Kituo cha Kudhibiti Magonjwa (CDC) nchini Marekani kinaripoti takwimu za kustaajabisha katika kila mtoto mmoja kati ya watoto 36 nchini Marekani amegundulika kuwa na changamoto ya usonji.

"Tafiti hiyo ilifafanua kwamba kati ya watoto 37 wa kiume mmoja wao huwa na changamoto ya Usonji. ‘’

“Zaidi, tafiti hiyo ilibaini kati ya watoto 157 wa kike mmoja wao hubainika na changamoto ya usonji hii inaonesha watoto wa kiume hupatwa na tatizo hili mara nne zaidi ya watoto wa kike. Kwa hapa Tanzania, takwimu zetu wenyewe zinaonyesha ongezeko kubwa la tatizo hili katika miongo miwili iliyopita, huu ni wito wa kuchukua hatua, wito wa kujibu kwa huruma, uelewa, na kwa hatua madhubuti.’’ Alibainisha.

Pia amesema Mkutano huo mkubwa Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambapo takribani nchi 20 ikiwemo Uingereza,India ,Uholanzi,Italia,Kenya,Umoja wa falme za Kiarabu, Afrika Kusini pamoja na nchi zingine.

Nae Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa taasisi ya (AUTISM CONNECT) Dolly Thakkar ameeleza kuwa ya mkutano huo wa siku mbili, ambao utakuwa na lengo la kuongeza ufahamu kuhusu usonji na kutoa jukwaa kwa wataalamu kutoka duniani kote kubadilishana uzoefu na kujadili maendeleo ya hivi karibuni kuhusiana na changamoto hiyo.

Thakkar ameeleza kuwa Mkutano huo kwa nchi ya Tanzania unakuwa ni mara ya kwanza ambapo awali ulifanyika dubai Aprili 2023. ambapo Mwezi Aprili ulifanyika Dubai na hivyo kwa Bara la Afrika ni Mara ya pili Mkutano huo mkubwa unaenda kufanyika.

Aidha ameeleza kuwa Mkutano huo utaruhusu mijadala mbalimbali kutoka kwa Madaktari bingwa pamoja na waongeaji nguli kutoka nchi tofauti tofauti.

Kwa upande wake Daktari wa Kipindi cha Afya check Dkt.Isac Maro amesema Mkutano huo mkubwa utaenda kubadilisha taswira zilizojengeka katika jamii kuwa hali hiyo ya Usonji ni hadi sasa haijajulikana tiba yake ya awali pindi Mama anapokuwa Mjamzito ili kuweza kumnusuru kuzaa mtoto mwenye hali ya Usonji.

"Tanzania tumepata Baraka kuwa wenyeji wa Mkutano huo wa Kimataifa wa hali ya Usonji ambapo wazazi wenye watoto wana Usonji wanaenda kukutana na Madaktari bingwa kutoka mataifa tofauti tofauti ili kuongeza maarifa na namna ya kulea watu wenye hali hiyo katika jamii zetu."

Ameeleza pia takwimu zinaonyesha kuwa Kati ya watoto 36 yupo mmoja anazaliwa na hali ya Usonji.


Pia ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kutafuta afua kukabiliana na watoto wenye hali hiyo mashuleni lakini bado sio rafiki sana katika kuwasaidia kuendelea kukuwa na kujifunza vitu mbalimbali.

 

Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa taasisi ya Autism Connect Bi Dolly Thakkar (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiani na ujio wa Mkutano wa Kimataifa unaolenga kujadili changamoto zinazohusiana na usonji na utindio wa ubongo utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Disemba mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam. Mkutano huo muhimu umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya taasisi ya Victorious Centre of Excellence na Autism Connect. Wengine ni pamoja na  Mkurugenzi wa taasisi ya Victorious Centre of Excellence Bi Sarah Laiser (kushoto) na  Mratibu mkutano huo Bi Lilian Mwasha (Kulia)
 

Mkurugenzi wa taasisi ya Victorious Centre of Excellence Bi Sarah Laiser (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiani na ujio wa Mkutano wa Kimataifa unaolenga kujadili changamoto zinazohusiana na usonji na utindio wa ubongo utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Disemba mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam. Mkutano huo muhimu umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya taasisi ya Victorious Centre of Excellence na Autism Connect. Wengine ni pamoja na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa taasisi ya Autism Connect Bi Dolly Thakkar (Kushoto) na  Mtaalamu wa Masuala ya Afya Dk Issack Maro (Kulia)

Share To:

Post A Comment: