Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Vyombo vya Habari wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa Maji uliondaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ya Ethiopia jijini Addis Ababa Ethiopia.
Katika Mahojiano hayo. Mhe Waziri ametilia mkazo umuhimu wa nchi mbalimbali duniani kutenga bajeti zaidi kwa ajili ya Sekta ya Maji kwa kuwa inagusa moja kwa moja jamii kama vile Sekta ya Afya.
Aidha, alisema kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Maji ili kuhakikisha kuwa malengo ya maendeleo endelevu yanafikiwa
Dkt. Nchemba alisisitiza kuwa jamii iliyoko vijijini inauhitaji mkubwa wa huduma ya maji kama ilivyo katika miji mikubwa ambapo ameeleza kuwa watu waondokane na dhana ya zamani kuwa vijijini wamepitiwa na mito na mabwabwa hivyo uhitaji sio mkubwa na kutaka fedha ziwe zinapelekwa kwa uwiano sawa.
Alisisitiza zaidi kuhusu umuhimu wa Sekta binafsi kuwekeza katika huduma za utoaji maji, akiongeza kuwa Serikali inaweza kutoa ruzuku kwa sekta binafsi katika uzalishaji ili uzalishaji uwe na tija na kuweza kufikia mahitaji ya idadi ya watu ambayo inakua kwa kasi.
Mhe. Dkt. Nchemba alisisitiza pia kuhusu umuhimu wa mifuko ya mazingira (Climate Funds) kutoa vipaumbele sawa kwa Sekta ya Maji kama vile inavyofanyika katika Sekta zingine ikiwemo nishati.
Post A Comment: