Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kuwa makini na majukumu yake baada ya kubaini maji yanayotoka katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe Yanarangi isiyoridhisha na si salama kwa matumizi ya wagonjwa.
Mahundi amepata pongezi hizo baada ya kuambatana na Waziri Mkuu akikagua majengo na yeye kuanza kukagua ubora wa maji na kubaini hayaridhishi na kutoa maelekezo kwa meneja Wa Maji Mkoa kuhakikisha anafunga vifaa vinavyochuja uchafu na maji yatoke yakiwa meupe kabla ya Tarehe 15Dec
Baada ya kutoa maelekezo hayo Mheshimiwa Mahundi, Waziri Mkuu ndipo alipobaini umakini wa kiongozi huyu na kumpa pongezi hadharani kwa kujiongezea kukuagua huduma ya maji.
Post A Comment: